Kamanda wa polisi mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni, Charles Kenyela akimvisha ubingwa wa Afrika Mashariki bondia Thomas Mashali baada ya kumpiga Bernad Mackoliech wa Kenya kwa KO
Na Elizabeth John
|
BONDIA Thomas Mashali juzi aliweza kuutetea ubingwa wa
Afrika Mashariki na Kati kwa kumtwanga kwa KO Mkenya Benard Mackoliech, raundi ya 6 katika pambano lililofanyika ukumbi wa
Friends Corner jijini Dar es Salaam.
Katika raundi
za mwanzo, Mackoliech alianza vizuri kitu kilichozua minong’ono
kwa watu, kwamba haiwezekani ubingwa uende nchi nyingine kabla ya raundi ya
tano Mashali kuzinduka.
Katika
mapambano ya utangulizi, Bakari Mohamed
alishinda kwa pointi dhidi ya Godfrey Musa
katika pambano la raundi nne, Amaduu
Mwalimu walitoka sare na Cosmas Kibuga, Mwaite Juma
akashinda kwa KO dhidi ya Frank Zagarino katika raundi ya tatu.
Pambano hilo liliendeshwa na
refarii Mark Hatia na majaji walikua ni Kulwa makaranga, Sakwe Mtulya
na Fidel Hynes.
Kwa mujibu wa Kamanda wa polisi Mkoa wa Kinondoni,
Charles Kenyela, ambaye alikua mgeni rasmi katika pambano hilo, tanzania kuna
vipaji vya ngumi hii ni furaha kwa watanzania wote kama ubingwa umeendelea
kubaki nyumbani.
“Nampongeza sana Mashali kwa kutwaa ubingwa huo kwa mara
nyingine.Tanzania tuna vipaji sana vya ngumi, hivyo tuendelee kukuza vipaji vya
hapa kwetu na sio kutoka nchi za wenzetu,” alisema Kenyela.
No comments:
Post a Comment