Mario Balotelli wa AC Milan akichuana na mchezaji wa Parma wakati wa mechi ya Serie A, Balotelli leo atakuwa dimbani wakati Milan itakapoumana na mahasimu wao Inter kwenye dimba la San Siro.
Hii ilikuwa mechi ya mzunguko wa kwanza wa Serie A, kati ya AC Milan na Inter Milan
MILAN,
Italia
Tayari makocha wa timu hizo pinzani
zinazotumia dimba moja la San Siro Massimiliano Allegri wa AC Milan na Andrea
Stramaccioni wa Inter wameingia katika malumbano na tambo kuelekea mtanange
huu, huku kila mmoja akikimwagia sifa kikosi chake
BAADA ya
kuwaduwaza FC Barcelona ya Hispania katika mechi ya kwanza hatua ya mtoano wa
16 bora wa Ligi ya Mabingwa Ulaya, AC Milan leo
inashuka tena katika dimba la nyumbani la San Siro kuwavaa mahasimu wao Inter Milan – katika pambano kali
la Serie A.
Ikiongozwa na
nyota wa zamani wa Inter, Mario Balotelli – ambaye hakucheza pambano Ulaya
dhidi ya Barca, Milan inatarajia muendelezo wa furaha kwa mashabiki wake, huku ‘mtukutu’
huyo (Balotelli) akitazamwa kwa jicho la tatu kama anaweza kuwaua nduguze hao.
Licha ya
kutarajiwa kuendeleza utikisaji nyavu alioanza nao tangu alipotua Milan akitokea Manchester
City ya England, Balotelli leo anatabiriwa
huenda akapata wakati mgumu dimbani, kutoka kwa mashabiki wake wa zamani ambao
hawajafurahishwa na ujio wake huo.
Wiki iliyopita
Inter ilipigwa faini kwa kumfanyia vitendo vya kibaguzi nyota huyo, ambaye
aliingia uwanjani hapo kutazama mechi ya Inter Milan
na Genoa, lakini akakumbana na kadhia hiyo baada
ya kuwaudhi mashabiki kwa kuvaa jezi za Milan.
Kama ilivyo kwa Milan, Inter nao wanaingia katika pambano hili ikitoka
kusonga mbele hatua ya 16 bora ya Europa League, baada ya kuichapa CFR Cluj
Napoka ya Romania
kwa mabao 3-0 na kuing’oa kwa jumla ya mabao 5-0 na sasa itaumana na Tottenham.
Tayari makocha
wa timu hizo pinzani zinazotumia dimba moja la San Siro Massimiliano Allegri wa
AC Milan na Andrea
Stramaccioni wa Inter wameingia katika malumbano na tambo kuelekea mtanange
huu, huku kila mmoja akikimwagia sifa kikosi chake.
Ukiondoa pambano
hilo, Sampdoria
itasshuka dimba la nyumbani kuwavaa Chievo, huku Atalanta ikitaraji kupimana
ubavu na AS Roma.
Bologna itakuwa na kibarua kipevu mbele ya Fiorentina,
Cagliari ikikabiliana na Torino, Juventus ikiwavaa
Siena na Parma kutunishiana
misuli na Catania.
SuperSport.com
No comments:
Post a Comment