Oscar Pistorius akiwa mahakamani
JO’BURG,
Afrika Kusini
Pistorius alilipa dhamana ya dola
113,0000, ikiwa ni pamoja na kukabidhi pasi yake ya kusafiria, kutakiwa kutoingia
katika nyumba yake iliyofanyikia mauaji jijini Pretoria na kuripoti kituo kikuu cha polisi
kila siku za Jumatatu na Ijumaa
KESI ya mauajia
inayomkabili bingwa wa mbio za walemavu ‘Paralimpiki’, Oscar Pistorius – inatarajiwa
kuanza kusikilizwa Juni 4 na sasa ataendelea kuwa nje kwa dhamana aliyopata
juzi Ijumaa.
Pistorius
aliachiwa juzi kwa dhamana, baada ya mahakama jijini Pretoria kuhakikishiwa kuwa nyota huyo hawezi
kukimbia, wala kufanya kitendo cha kihalifu na kwamba apewe dhamana ili
ajipange kukabiliana na mashtaka.
Tayari Pistorius,
26, alishayakana mashitaka ya kuua kwa kukusudia, akisema alimpiga risasi mpenziwe
Reeva Steenkamp, 29, kwa bahati mbaya, baada ya kuhisi likuwa amelala wakati
alipokuwa akishambulia mlango wa bafu kwa risasi.
Pistorius
alitumia jumla ya siku nane akiwa kuzuizini jijini Pretoria, tangu alipokamatwa na kuwekwa ndani
Februari 14 (Siku ya Wapendanao) aliyofanya tukio – hadi juzi Ijumaa
alipodhaminiwa.
Baada ya dhamana
yake Ijumaa, Pistorius aliondoka mahakamani hapo akiwa ndani ya gari maalum la
rangi ya Silva, huku akifuatwa na wapiga picha za video na mnato kutoka vyombo
mbalimbali vya habari duniani.
Mwanamichezo
huyo kipenzi cha wengi, hakuelekea nyumbani, badala yake alipelekwa nyumbani
kwa mjomba wake – ingawa ni katika jiji hilo hilo la Pretoria.
Ripoti zinasema
kuwa, huenda Pistirius akaanza rasmi mazoezi baada ya kurejea uraiani, ikiwamo
kuzungumza kwa mara ya kwanza na mkufunzi wake, ingawa awali wakala wake
alitangaza kufuta ratiba yote ya mwanariadha.
Hakimu Desmond
Nair alikubali opmbi la dhamana ya Pistorius kutoka kwa wanasheria wanaomtetea,
ambapo alidhaminiwa kwa kiasi cha pauni 74,000 (sawa na dola 113,000).
Pistorius aliamuriwa
sambamba na dhamana hiyo, kukabidhi pasi yake ya kusafiria, kutoingia katika
nyumba yake iliyofanyikia mauaji jijini Pretoria
na kuripoti kituo kikuu cha polisi mara mbili kwa wiki katika siku za Jumatatu
na Ijumaa.
BBC
No comments:
Post a Comment