HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

February 09, 2013

MAZISHO YA ASKOFU LAISER KUFANYIKA IJUMAA FEBRUARI 14

S
Askofu Laiser siku za mwisho za uhai wake. Hapa alikuwa hospitali ya rufaa ya Seliani iliyopo jijini Arusha ambako alikuwa amelazwa kwa siku kadhaa akipata matibabu. Kulia ni Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, akimjulia hali. (Picha kwa Hisani ya JamiiForum.com)
 Marehemu Thomas Laiser enzi za uhai wake

Aliyekuwa Askofu Mkuu wa KKKT Kanda ya Dayosisi ya Kaskazini, Thomas Laizer (kulia) enzi za uhai wake akitekeleza majukumu yake. Hapa alikuwa anauombea mwili wa aliyekuwa muhasisi wa chama cha NCCR Mageuzi katika ibada ya kumuombea iliyofanyika katika Kanisa la OLigilai. (Picha kwa Hisani ya Libeneke la Kaskazini Blog)
 Marehemu Askofu Thomas Laiser

ARUSHA, Tanzania

Waumini na Washirika wa Kanisa Kuu na makanisa yote ya KKKT nchini, wananchi, ndugu, jamaa na marafiki watapata fursa ya kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu kuanzia Alhamisi Februari 14, alasiri
MAZISHI ya aliyekuwa Askofu wa Kanisa la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Kaskazini Kati, Marehemu Askofu Thomas Laizer, yanatarajiwa kufanyika Ijumaa Februari 15, 2013.

Kwa Mujibu wa Taarifa maalum iliyotolewa na Kamati ya Mazishi ya KKKT na familia ya Laiser, inasema kuwa, marehemu atazikwa katika eneo la Kanisa Kuu Mjini Kati, Arusha.

Taarifa hiyo imeongeza kuwa, Waumini na Washirika wa Kanisa Kuu na makanisa yote ya KKKT nchini, wananchi, ndugu, jamaa na marafiki watapata fursa ya kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu kuanzia Alhamisi Februari 14, alasiri.

Pia, taarifa hiyo ya kamati/familia iliongeza kuwa, mwili wa Askofu Laizer utalala Kanisani hapo hadi Ijumaa ya mazishi.

Marehemu Laizer alizaliwa Machi 10, 1945 katika Kijiji cha Kitumbeni mkoani Arusha na kupata elimu yake ya msingi hadi darasa la nane katika shule ya Longido, alikkomaliza mwaka 1965.

Marehemu wakati wa uhai wake alikuwa Mwinjilisti, Mchungaji katika makinisa mbalimbali nchini na baade kuwa Mkuu wa Jimbo na Mkuu wa Sinodi, kabla ya kutawazwa kuwa Rais wa sinodi na kisha kusimikwa rasmi kuwa Askofu wa Kwanza wa Dayosisi ya Arusha, (sasa Dayosisi ya Kaskazini Kati).

Bwana alitoa, bwana ametwaa, jina lake lihimidiwe. Ameen.

No comments:

Post a Comment

Pages