HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

February 09, 2013

MAOFISA HABARI WA SERIKALI WAMALIZA KIKAO CHAO DODOMA, WATEMBELEA BUNGE NA KUSHIRIKI UPANDAJI WA MITI UDOM

Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari Raphael Hokororo akiwafundisha Maofisa Habari na Mawasiliano  wa Serikali kutoka Wizara, Taasisi, Wakala na Mashirika ya Umma, Mikoa na Wilaya upigaji wa picha bora  za mnato kwa  matumizi ya habari wakati wa kuhitimisha kikao cha maofisa hao mjini Dodoma. (Picha zote na Aron Msigwa - Idara ya Habari MAELEZO)
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Clement Mshana ambaye alikua miongoni mwa waalikwa waliohudhuria kikao kazi cha Maofisa Habari na Mawasiliano wa Serikali, akiongea na maofisa hao mjini Dodoma.
 Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Sihaba Nkinga, akizindua zoezi la upandaji wa miti lililowahusisha Maofisa Habari wa Serikali katika Kampasi ya Chuo Kikuu Dodoma (UDOM).
 Maofisa Habari na Mawasiliano wa Serikali wakiendelea na zoezi hilo Chuo Kikuu cha Dodoma.
 Mhasibu Mkuu Msaidizi wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Swalehe Chondoma akishiriki zoezi la upandaji wa miti katika kampasi ya Chuo Kikuu cha Dodoma.
 Maofisa Habari na Mawasiliano wa Serikali wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kutoka nje ya Ukumbi wa Bunge mjini Dodoma.
Maofisa Habari na Mawasiliano wa Serikali wakiwa ndani ya Ukumbi wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mjini Dodoma baada ya kupata mwaliko wa Spika wa bunge hilo, Anne Makinda na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk Fenella Mukangara.
Maofisa Habari na Mawasiliano wa Serikali wakiwa wamesimama kwa utambulisho ndani ya Ukumbi wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mjini Dodoma.
 Maofisa Habari na Mawasiliano wa Serikali wakiwasili Chuo Kikuu cha Dodoma kushiriki zoezi la upandaji wa miti chuoni hapo ikiwa ni sehemu ya mchango wao katika kuhifadhi mazingira ya chuo hicho.
Baadhi ya viongozi wa Idara ya Habari (MAELEZO), Mkurugenzi wa Idara hiyo Assah Mwambene (wa nne kutoka kushoto) na Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Habari Usajili wa Magazeti, Raphael Hokororo (wa pili kutoka kushoto) wakiwa wamesimama ndani ya ukumbi wa Bunge kuwasalimia waheshimiwa wabunge mara baada ya kuombwa kufanya hivyo na Spika Makinda.
Baadhi ya Maofisa Habari na Mawasiliano wa Serikali wakiendelea na zoezi hilo Chuo kikuu cha Dodoma.

1 comment:

  1. Have you ever thought about publishing an e-book or guest authoring on other blogs?
    I have a blog based on the same ideas you discuss and would love to have you share some stories/information.
    I know my audience would appreciate your work. If you're even remotely interested, feel free to shoot me an email.

    Here is my web site :: Amelia Island Plantation Vacation Rentals
    Here is my web-site : internet affiliate marketing

    ReplyDelete

Pages