Na. Bryceson Mathias
KWA Tanzania Mlima Kilimanjaro, Hifadhi ya Ngorongoro na Hifadhi ya Serengeti, si maajabu, ila maajabu ni Mwanafunzi nchini kufaulu Mtihani wa Shule ya Msingi kwenda Sekondari akiwa hajui Kusoma, Kuandika na Kuhesabu.
Wakati Serikali na wadau fulani wakitumia fedha nyingi kuwarubuni na kuhamasisha kuyapigia yanayoitwa maajabu ya Afrika Mlima Kilimanjaro, Hifadhi ya Ngorongoro na Hifadhi ya Serengeti , maajabu ya watoto kufaulu mtihani wakati hajui kusoma, kuandika na kuhesabu yanapuuzwa na kuwekewa mikingamo.
Bado sipati picha ni kipi kizuri na kipaumbele cha kwanza chenye tija kwa familia yako, kuwakaribisha wageni watakaokuja mikono mitupu na kula chakula cha watoto wako, na halafu wakitoka wanachukua Masufuria, Unga na mboga kidogo uliyobakiwa nao, Vyombo na miiko ya kupikia?.
Mtu asiyeamini hapa anaweza akawa ni mtu anayechangia Mlima Kilimanjaro usiosema, usioona Njaa, usiotaka mavazi, usitaka mahali pa kulala, usiotaka elimu, Matibabu, maana tayari Mungu aliupa Malazi ya Kilimanjaro, Nguo za Miti na Majani yenye Rangi nzuri, Theruji chakula cha Udongo.
Mtu mwenye Utu, Utaifa, Uzalendo na Fikra za kifamilia hawezi kuwaacha watanzania waliohoi kwa maisha magumu na kero zisizoisha, akahamasisha kuchangia Mlima Kilimanjaro, Hifadhi ya Ngorongoro na Serengeti kwanza badala ya watu.
Mtu wa namna hiyo, akiwaacha wanafunzi wafeli asilimia 60%, waongoze kwa alama za Ziro, huku maeneo mengine wananchi wakisurubishwa na njaa wakishindia na kulalia majani ya mboga na wadudu wa kumbikumbi, Biblia inamuita huyo ni mtu asiyeamini, Mpangani wa Utu, Maendeleo wa Mwili na Roho.
Watu wa namna hiyo, ndio wanaofadhiri na kuwatumia viJana kwa kutokujua kama Karai la Zege kuwajeruhi na kuwaua viongozi wa Dini Mashekhe, Mapadre, Wachungaji na kuharibu nyumba za Ibada na Samani zake, na baadaye kudharau kama Karai likimaliza kujenga Nyumba, hutupwa nje bila chochote!!.
Hatuoni maajabu ya watu kuwa mbuga za Wanyama kama Ngorongoro, Mbuga zimefurika Wanyama, Rutuba ya Ardhi lakini wananchi wakabiliwa na njaa kiasi cha kutaka kupoteza maisha ya watu? Itakuwaje mtu achunge na kukamua Ng’ombe azuiwe asinywe maziwa? Mpakuaji Asali asile?
Hii haina tofauti na kukubali vyama Vingi halafu hutaki vyama vifanye mikutano, ulikubali viwepo vya nini kama hutaki vifanye mikutano? Ukikubali kuzaa watoto ukubali na kuwalisha na kuwahudumia kwa muda wote wa utoto wao hadi wakomae wajitegemee, usipofanya hivyo wakijua mema na mabaya!.....
Ieleweke mimi sipingani na kuchangia maajabu hayo kwa wale wanaotaka tupate maendeleo ya kweli ili yawasaidie watanzania kujikwamua kutoka hapa tulipo kwenda mahali pengine, lakini ninachokikataa ni pale ambapo Viongozi kama Kiti cha Spika, Naibu wake na wanaowasaidia, wanapokanyaga Kanuni na kuturudisha kwenye Analogia wakati tuko Digitali; Huko tumetoka!!
Ninachokikataa ni pale ambapo watu wanatung’ang’aniza walalahoi tununue kwa nguvu ving’amuzi vya Startimes ambavyo kwa Kauli za Viongozi wa Chadema katika Mkutano wa uliofanywa Jumamosi Februari 23, 2013 Mwanga Bar, vimekataliwa na nchi za majirani zetu eti tu vina mkono wa Kigogo.
Ninachokataa ni kuturejesha kwenye Analogia ya vithibiti mwendo (Speed Governor) vilivyoshindwa au kuwarejesha wazee waliostaafu waongoze vyama, Serikali na wananchi ambao wako Digitali yeye akiwa bado yuko kwenye ndoto za Adamu na Hawa. Huwezi kusema umeng’atuka uongozi halafu ukasema unarejea.
Tabia ya kurejea rejea kwenye uongozi ukingatuka, ni Uroho na Uchoyo amabao ni sawa na kuvimbiwa , ambapo madhara yake ni kuharibu hali ya Hewa kunakotokana na Ulafi ambao mwisho wake humfanya mtu atapike.
Aidha Kitendo hicho ni sawa kula matapishi yako,kwa sababu ukirejea kwenye uongozi utapelekeshwa, utalala usingizi na kuwapa nafasi Nzi wakuingizie uchafu mdomoni wa, Rushwa, Ufisadi na Umangimeza halafu utauugua bure!! Na wewe hali umezeeka. Huo ni mwanya mbaya wa kukufanya uharibu vitu halafu upoteza heshima yako iliyojengeka kwa gharama, na matokeo yake utadharauliwa.
Hivyo waachieni vijana mbaki mkiwashauri kuipeleka Tanzania mahali pazuri, badala ya kuthamini kuondoa maajabu, ambayo mwanafunzi anafaulu Shule ya Msingi na kwenda Sekondari, wakiwa hawajui kusoma, Kuandika na Kuhesabu, huku Mawaziri wa wizara husika wanang’ang’ania kuongoza katika Janga na Msiba huo; Kama mimi ningekuwa Kawambwa, Mulugo na Mtendaji wa Juu Elimu, ningejiuzulu.
0715-933308
No comments:
Post a Comment