HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

February 24, 2013

Wakaguzi waliofichua ubadhirifu Mil. 585/- Mvomero, mashakani kutimuliwa


Emmanuel Gabriel Chambo (kulia) Mjumbe Mpya wa Halmashauri ya Kijiji cha Mlaguzi 

Na Bryceson Mathias, Mvomero Morogoro

WAKATI Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mvomero Jonas VanZealand akisema Baraza la Madiwani wilayani humo halipo tayari kufanya kazi na Mkurugenzi Sala Linuma kutokana na Ubadhirifu wa Mil. 585/- kwa miezi 8 tu, Wakaguzi wa ndani waliofichua uozo huo wako mashakani kutimuliwa.

Tuhuma hizo zimebainika jana kufuatia kuwepo kwa sekeseke la baadhi ya vigogo wanaoonekana kumkumbatia Mkurugenzi huyo asing’olewe, baada ya madiwa hao kumwandikia waraka Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Joel Bendera ya kuondokewa na Imani na Utashi wa kufanya kazi naye.

Uchunguzi uliofanywa kwa nyakati tofauti hili toka kwa cvyanzo vyetu ndani ya Halmashauri hiyo vimebainisha kwamba, mbali ya Barua hiyo Kumb. MVDC/CPF.49/14 ya 10/2/2013 ya kumkataa mkurugenzi inadaiwa kwamba, wakaguzi wa ndani waliofichua uovu huo, wanafanyiwa mizengwe ili watimuliwe.

“Pamojana kufanya kazi nzuri ya kubaini na kuweka wazi ubadhirifu huo, tuna changamoto toka kwa vigogo wanaomkumbatia mkurugenzi huyo ambaye kihistoria kwa wakati wake kumekuwa na mfurulizo wa ubadhirifu wa miradi vijijini ukiwemo wa Zahanati ya Kijiji cha Mlaguzi zaidi ya Mil. 300/-.alisema akiomba asitajwe.

Wakaguzi hao wameonya kuwa watafichua mambo ya kutisha zaidi iwapo Vigogo hao watathubutu kuwatumia kama Kondoo wa Sadaka kwa Lengo la kumbeba Mkurugenzi huo ambaye ameshatoboa Mbeleko ya kumbebea kutokana na ubadhrifu huo, yakiwemo madai ya Mil. 10/- kutumika kwa Harusi.

Wakitolea Mradi wa Zahanati Mlaguzi Kata ya Sungaji ambao uliliripotiwa kuwa uko kwenye hatua ya Lenta, wakati kiukweli uko kwenye Msingi kama unavyoonesha kwenye (Picha walisemaa, takribani zaidi ya Mil. Tano zimemenmg’enywa na kuzibwa kwa Taarifa za Uongo.

Aidha Mkuu wa Mkoa Bendera baada ya kupokea Malalamiko yaMadiwani kupitia kwa Mwenyekiti wa Halashauri ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Diongoya Zealandi aliyetishia kuacha Udiwani na Uenyekiti wa Halmashaurii, kama Tume aliyounda Bendera itadiriki kufanya kazi  Mkurugenzi akiwa kazini, jambo lililoungwa mkono na Wakaguzi hao, Madiwani na wadau mbalimbali wilayani mvomero, na badala yake wanataka awe nje ili apishe asishawishi wala kuiongoza tume ikifanya uchunguzi huo.

No comments:

Post a Comment

Pages