LONDON, England
Arsene Wenger amewataka nyota wake kusahahu kilichotokea
katika Kombe la FA na kuanza harakati mpya za kuweka hai matumaini ya kutwaa
kombe msimu huu kwa kuwalaza Bayern – ambao msimu uliopita walifungwa fainali
na Chelsea
WANAFAINALI wa msimu uliopita wa Ligi ya Mabingwa Ulaya,
Bayern Munich ya Ujerumani, leo inajitupa ndani ya dimba la Emiartes jijini
hapa kuwavaa wenyeji wa Uwanja huo, Arsenal katika mechi kali ya mtoano wa 16
bora wa michuano hiyo.
Arsenal, ambao wamefanikiwa kutinga hatua hii kwa mara ya 13
sasa, ina kibarua kigumu cha kupoza machungu ya mashabiki wao, wanaougulia
kichapo kilichowang’oa katika michuano ya Kombe la FA ilipowaalika nyumbani
Blackburn Rovers.
Kocha wa Gunners, Arsene Wenger amewataka nyota wake
kusahahu kilichotokea katika Kombe la FA na kuanza harakati mpya za kuweka hai
matumaini ya kutwaa kombe msimu huu kwa kuwalaza Bayern – ambao msimu uliopita
walifungwa fainali na Chelsea.
“Tunapaswa kusahau kilichotokea dhidi ya Blackburn. Tugeuzie
umakini wetu dhidi ya Bayern ili kuona ni kwa namna gani tunachanga vema karata
kuelekea robo fainali.
“Tunacheza nyumbani na tunapaswa kuwapoza mashabiki wetu kwa
kushinda,” alisema Arsene Wenger aliyesisitiza kutokuwa na mpango wa kujiuzulu
licha ya kufeli kwa majaribio yake ya kutwaa taji kwa miaka minane sasa.
Aidha, mshambuliaji Lukas Poldoski, amewakumbusha nyota
wenzake kuweka hofu kando na kujiamini wakati huu wanapoivaa Bayern: “Hatuna
haja ya kuihofia Bayern. Ni timu nzuri yenye nyota wa kiwango cha juu, lakini
tuna uwezo wa kuwafunga na kuhakikisha tunawang’oa jumla mashindanoni.”
Ukiondoa pambano la Arsenal na Bayern Munich, leo pia
kutakuwa na mechi kati ya mabingwa wa michuano hii mwaka 2004, FC Porto ya
Ureno itakayoshuka dimba la nyumbani la Estadio do Dragao, jijini Porto Ureno,
kuwaalika Malaga ya Hispania.
Pambano hili linatarajiwa kujaa ushindani, kutokana na soka
la Porto na kiwango kilichooneshwa na Malaga msimu huu, ambayo imezika jinamizi
la ukata uliokuwa ukiikabili na kulazimika kuwauza nyota wake na kushangaza
wengi hatua ya makundi kwa kufuzu mtoano huu.
……SuperSport.com……
......SCHWEINSTEIGER: USHINDI LAZIMA LEO
MUNICH, Ujerumani
‘Tunasema kwa Kijerumani, “Mia san mia” – ikimaanisha
“Sisi ndio sisi.” Kauli hiyo haitufanyi sisi kuwa kiburi, bali utupa kujiamini
na kuchagiza ushindi mchezoni. Inahusu zaidi kuongeza morali wa ushindi akilini
mwetu”
KIUNGO wa kimataifa wa Ujerumani na klabu ya Bayern Munich
ya hapa, Bastian Schweinsteiger, amesema kushinda pambano lao leo dhidi ya
Arsenal ndio ‘mpango mzima’ na kuwa ubora wa soka la kitabuni kwao halina tija.
'Katika Bayern Munich, tunacheza ili kushinda,’ alisema
Schweinsteiger akiwa buheri wa afya kwenye sofa za kitambaa chekundu
zinazopamba vyumba vya kuvalia vya Uwanja wa Allianz Arena, akibainisha nia ya
kuiondosha Gunners na kutinga robo fainali.
Schweinsteiger anaongeza: ‘Kuna kauli mbiu maarufu mno
miongoni mwa wakazi wa hapa Bavaria na ambayo tumekuwa tukiitumia sisi ndani ya
Bayern Munich.
‘Tunasema kwa Kijerumani, “Mia san mia” – ikimaanisha “Sisi
ndio sisi.” Kauli hiyo haitufanyi sisi kuwa kiburi, bali utupa kujiamini na
kuchagiza ushindi mchezoni. Inahusu zaidi kuongeza morali wa ushindi akilini
mwetu.
‘Wakati wachezaji wanapokuja hapa kutoka sehemu nyingine,
mara kadhaa wao huonesha furaha tunapomaliza mechi kwa sare ya 0-0 au 1-1,
lakini sisi tuliokulia katika mazingira ya hapa, hatufurahii kitu kama hicho
zaidi ya ushindi.
‘Sisi kamwe haturidhiki na matokeo ya sare ya 0-0 au 1-1.
Hilo liko mawazoni mwa kila mmoja miongoni wa Wajerumani, hususani wa klabu hii
ya Bayern Munich,’ alisema Schwenisteiger akionekana hatanii.
……Daily Mail…….
Mwisho
RATIBA MABINGWA ULAYA
LEO JUMANNE FEBRUARI 19
Arsenal v Bayern Munich – Emirates, saa 4:45
FC Porto v Malaga - Estadio do Dragao, saa 4:45
KESHO JUMATANO FEBRUARI 20
AC Milan v Barcelona - San Siro, saa 4:45
Galatasaray v Schalke - Turk Telekom Arena, saa 4:45
VINARA WA MABAO MABINGWA ULAYA
Mchezaji Timu Mabao
C. Ronaldo Real
Madrid 7
B. Yilmaz Galatasaray 6
Oscar Chelsea 5
Lionel Messi Barcelona 5
Osorio Alan Braga 5
Lewandowski Dortmund 5
Willian Shakhtar 4
Ez. Lavezzi PSG 4
Jan Huntelaar Schalke
4
K. Mitroglou Olympiacos 4
No comments:
Post a Comment