HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

February 08, 2013

Tukiwa na Madiwani 29 aina ya Awadhi, Mil. 27/- zingesalimika


 Moja ya Uchafu ulioko mkoani Dodoma Kata ya Kikuyu ambao hauhitaji ziara ya kwenda Mwanza au Elimu ya Ziada ili kuutoa.


Na Bryceson Mathias
 
TUKIWA na Madiwani 29 tu; sawa na Diwani mmoja kwa kila Mkoa wenye tabia na uchungu wapata wananchi wa namna ya Awadhi Abdallah (CCM) Kata ya Zuzu,  Halmashauri ya Dodoma, Ufisaji nchini ungekwisha na kufa kifo cha Mende na Mil. 27/- za ufujaji kama ule wa Dodoma; fedha zake zingesalimika..
 
Hivi karibuni Diwani Abdalah , alipinga na kukataa kushiriki ziara ya siku tano ya kutembelea Jiji la Mwanza kujifunza usafi kwa gharama ya Mil. 27/- wakati wananchi wake wanateseka na kero mbalimbali zisizo na majibu, ambapo amehoji zingeweza kutengeneza madawati managapi?
 
Mbali ya Ufisaji kufa; nchi ingekuwa na maendeleo makubwa ambayo yangeweza kulifikisha Taifa hili kuweza kusomesha wanafunzi toka awali hadi vyuo vikuu bure, na kutupilia mbali gharama kubwa za bidhaa za ujenzi, Saruji na Mabati, ili wananchi wajenge nyumba bora.
 
Ujasiiri kama wa Diwani Abdalah ambaye alipinga kwa vitendo Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma, ambao walipitisha Bajeti ya zaidi ya sh Mil. 27/- kwa ajili ya ziara ya siku tano ya kutembelea Jiji la Mwanza kujifunza usafi huku wananchi wakiwa na hali mbaya kimaisha, hao ndio tungewataka wawakabe wabunge wanaolala mjengoni nchi isimalizwe.

Ingawa najua kwa Kitendo cha Diwani Abdalah kujitoa Mhanga na kurushia Makombora Madiwani na Uongozi wa Halmashauri ya Manspa ya Dodoma kwa kile kinachoitwa kufuja Mil. 27/- kitamgharimu kiasi cha kuundiwa mizengwe hata pengine kutaka kung'oa Udiwani kwa namna na yoyote ile. sina shaka wananchi wa Kata ya Zuzu hawakubali kuitwa Mazuzu, watakuwa na msimamo wa kupembua Pumba na Nafaka 2015 hata kwa kuona upande wa Pili wa Mil. 27/- hizo.
 
Hata hivyo baadhi ya Madiwani walisema, fedha zilizotengwa kwa lengo la kufanya ziara hiyo, zingeingizwa katika sekta ya maendeleo kama vile Elimu na Afya zingekuwa na tija zaidi kuliko kuzifuja kana kwamba zimetumbukizwa chooni kusikokuwa na mwenyewe.
 
Mustakabali huo ulisababisha baadhi ya madiwani kugoma kuungana na wenzao wakidai kufanya ziara hiyo ni kushiriki katika ufisadi wa mali ya umma, huku Mkoa huo (Dodoma) ukiwa unaongoza kwa Ombamba, Wazee, na watoto wa mitaani wanaokosa hata mlo wa siku moja.
 
Bajeti hiyo inaonesha kwamba kila Diwani atalipwa sh Laki Nne sawa na sh 80,000 kwa siku katika siku tano watakazokuwa jijini Mwanza, ambapo zinaweza kukarabati au kujenga upya Jengo la Chikande ambalo wajawazito hujigonjeleza ili wajifungue lenye hali mbaya kiafya.
 
Diwani Awadhi; “ ni ziara ngapi zimefanywa lakini hakuna maendeleo yoyote? Huku  ni kutaka kutumia vibaya fedha ya umma bila kuwahurumia wananchi wanaokosa hata kula mlo mmoja. Wenzangu wamebisha kwa maneno mimi nafanya kwa matendo siendi safari kabisa.
 
“Siwezi kushiriki katika ufisadi mkubwa kama huu, kila Diwani kapewa kiasi cha sh Laki nne kwa ajili ya siku tano, sasa jiulize kwa hesabu hiyo ya Mil. 20/- ni madawati mangapi?”.alisema abdalah.
 
“Kama suala ni kutembea na kujifunza, ni kwa nini asiitwe mtaalamu kutoka Mwanza ambaye angeweza kugharamiwa fedha kidogo ili akaendesha mafunzo jambo ambalo lingekuwa rahisi kufanya hata vitendo?” alihoji.
 
Diwani wa Kata ya Dodoma Makulu, Ally Bilingi (CHADEMA) alisema kuwa pamoja na kuwepo kwa safari nyingi za kujifunza mambo mbalimbali kama usafi na ukusanyaji mapato, bado hakuna tija yoyote ambayo imeijitokeza zaidi ya fedha nyingi kupotea bila sababu.
 
Kauli ya wapiga kura na Walipa kodi wa Mkoa wa Dodoma wanasema, fedha ambazo zitatumika kwenye safari hiyo ni kubwa mno hasa kutokana hali ya kimaisha ya wananchi wa kata wanazoongoza kuwa na changamoto mbalimbali.
 
“Kata nyingine hazina Maji Safi, Zahanati, Vituo vya Afya, Madawa, Madawati, ambapo wengina kwenye vijiji na vitongoji vitongoji vya Kata zao, hawana hata Ofisi ya Mwenyekiti wa Serikali ya Kitongoji, Kijiji na Hata Kata”.
 
Akimuunga mkono Abdalah, Diwani wa Kata ya Dodoma Makulu, Ally Bilingi (CHADEMA) alisema kuwa pamoja na kuwepo kwa safari nyingi za kujifunza mambo mbalimbali kama usafi na ukusanyaji mapato, bado hakuna tija yoyote ambayo imeoneka zaidi ya fedha nyingi kupotea bila sababu.
 
 

No comments:

Post a Comment

Pages