HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

February 24, 2013

Waziri Prof. Maghembe akumbuka Shuka kumepambazuka


Na Bryceson Mathias

Ni Mtazamo wangu kwamba, WazirI wa Maji Profesa Jumanne Maghembe amekumbuka Shuka kukiwa kumekucha, Ingawa amezitaka Mamlaka za Usambazaji maji safi na maji taka  jijini  Dar es Salaam (DAWASCO) na Pwani (DAWASA) kuhakikisha  tatizo la  wizi  wa  maji linakomeshwa na kuonya wafanyakazi atafukuzwa kazi.
 
Prof. Maghembe alisema hayo jana alipozungumza na wafanyakazi hao akidai jumla ya maji lita mil 300 zilizokusudiwa kusambazwa vyanzo vikuu, kwa utaratibu mbovu asilimia 56% zilipotea ambapo asilimia 30% na kudai wanaoibadai wanawajua na kuwafahamu wezi hao.
 
Ninasema Prof. Maghembe amekumbuka shuka kukiwa kumepambazuka kwa sababu anawakemee watendaji kuwa waache wizi badala ya kuwachukulia wakati mambo yameshaharibika, hasa kutokana na anachosema wahujumu wa maji wanajulikana.
 
Mambo anayofanya waziri huyo ingawa yanaonekana kuwa na sura ya kujikosha, kimsingi yanaendelea kumuumbua na kumfanya aonekana kwamba anakurupuka, kufuatia na shinikizo la Hoja binafsi ya Mbunge wa Ubungo John Mnyika,  kuonekana kama inamtafuna.
 
Makali ya Prof. Maghembe yalikuwa hivi, “Nataka muwe wazalendo katika kuwatendea haki wananchi kwa kuwapa maji badala ya kuwasambazia rafiki zenu wauza maji ili mpate mshiko,nikigundua kuna sehemu maji hayakupelekwa meneja husika na wafanyakazi wake nitawafukuza kazi papo hapo”alisema.
 
Licha ya kujitetea kuwa kuna uchakavu wa miundombinu inayosababisha maji kupotea pia alizitaja sababu nyingine kuwa ni pamoja na  mgawo wa upelendeleo  unafanywa na baadhi ya viongozi  katika kusimamia maji hayo wenye nia ya kujipatia chochote, lakini akasahu udhaifu wa usimamizi na uwajibika wa Ofisi yake.
  
Prof. Maghembe mbali ya kudai baadhi ya watendaji wanashirikiana na wauza maji kuwafungia mitambo akitolea mfano wa Mkwajuni kuliko na mfanyabiashara anayesambaza maji hadi  eneo la Mwanyamala wakati mitambo hiyo ilishaondolewa! Alishangaa kuiona imefungwa tena hadi juzi.
 
Hata hivyo ukweli halisi niuliopo ni kwamba, Bomba la eneo la Mkwajuni ni kubwa mno kiasi Mlalahoi hawezi kufunga mitambo, lakini pia kuna mitambo 10 katika maeneo hayo ambayo nayo wanaiba maji, jambo alilowashukiwa kuwa kwa mazingira hayo watendaji kwa namna yoyote wanahusika na uhujumu maji akiimba kuwachukuliwe hatua lakini hafanyi!!.
 
Pamoja na Prof. Maghembe kuwarushia mpira Wenyeviti wa mashirika hayo,  alitaka wahakikishe watu wote wanaouza maji  na malori wanajiandikisha na kutambuliwa  kisheria na DAWASCO, na maji wanayoyauza yawe safi, na wawe na Mita , Leseni  , Namba ya Mlipa Kodi, na pia bei ya kuuza  Maji idhibitiwe na EWURA, mambo ambayo yangefanywa hivyo mapema aibu hiyo isingekuwepo.
 
Ingawa alitaka zoezi hilo lianze  mara moja kuanzia  Mwezi Machi ili hadi April 30, mwaka huu  zoezi hilo liwe limekamilika, hayo yangelifanyika hivyo tangu awali na kukubali ushauri wa Mbunge wa Ubungu Mnyika “Chadema”, wizi wa maji unefikia asilimia 0%, hata mabwana maji wanaofanya vituko wasingekuwepo.

Aidha sipengi wazo la waziri la kutaka wananchi na wafanyakazi kuwataja wezi, kwa lengo atakayemtaja mharifu wa maji azawadiwe Sh.100,000/-, lakini hatua hiyo imechelewa kwa sababu imekuja baada ya kusukumwa na hoja tofauti tofauti kama hali ilivyo sasa, ingefanywa kwa uwajibikaji kabla ya Jogoo kuwika ingekuwa na tija.
 
 
0715-933308.

No comments:

Post a Comment

Pages