HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

March 05, 2013

MAKAMU WA RAIS AWEKA JIWE LA MSINGI UKARABATI WA BARABARA YA NYAGUGE-MUSOMA

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiongozana na Mbunge wa Butiama Vijijini, Nimrod Mkono, baada ya kusikiliza maelezo kutoka kwa Eng. Sabyasachi Kar, kuhusu mashine za kusaga mawe wakati alipotembelea kuona mashine hizo, zilizopo Kijiji cha Sabasaba Irimba, wakati akiwa katika ziara yake ya siku mbili mkoani Mara, iliyo sambamba na Uwekaji jiwe la Msingi ukarabati wa Barabara ya Nyaguge-Musoma, sehemu ya kutoka Mpaka wa Mikoa ya Simiyu na Mara hadi Musoma.

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, mkewe Mama Asha Bilal na Waziri wa Ujenzi, Dkt. John Pombe Magufuli, wakifurahia burudani ya ngoma ya asili, wakati walipowasili eneo la kuweka Jiwe la Msingi ukarabati wa Barabara ya Nyaguge-Musoma, sehemu ya kutoka Mpaka wa Mikoa ya Simiyu na Mara hadi Musoma, leo.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Waziri wa Ujenzi, Dkt. Jhn Pombe Magufuli, wakifurahia burudani ya muziki wa dansi kutoka kwa bendi ya Msondo Ngoma, wakati walipowasili eneo la kuweka Jiwe la Msingi ukarabati wa Barabara ya Nyaguge-Musoma, sehemu ya kutoka Mpaka wa Mikoa ya Simiyu na Mara hadi Musoma.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal na mkewe Mama Asha Bilal, wakifurahia vazi la Jadi baada ya kukabidhiwa na mzee wa Mkoa wa Mara, Thomas Sura, wakati wakiwa katika ziara yao ya siku mbili mkoani Mara na kuweka Jiwe la Msingi ukarabati wa Barabara ya Nyaguge-Musoma, sehemu ya kutoka Mpaka wa Mikoa ya Simiyu na Mara hadi Musoma, leo.
 Ilikuwa ni burudani ya kutosha kutoka kwa kikundi hicho.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Waziri wa Ujenzi, Dkt. John Pombe Magufuli na Mkuu wa Mkoa wa Mara, John Gabriel Tupa, kwa pamoja wakifunua kitambaa kuashiria uwekaji wa Jiwe la Msingi ukarabati wa  Barabara ya Nyaguge-Musoma, sehemu ya kutoka Mpaka wa Mikoa ya Simiyu na Mara hadi Musoma.

No comments:

Post a Comment

Pages