HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

March 05, 2013

MANCHESTER CITY, ILIVYOIDUNGUA ASTON VILLA BAO 1-0 VILLA PARK

 Edin Dzeko wa Manchester City (kushoto), akiwania kupiga mpira wa kichwa na Ciaran Clark wa Aston Villa, wakati wa mechi ya Ligi Kuu ya Uingereza iliyofanyika kwenye dimba la Villa Park na kwisha kwa City kushinda bao 1-0 lililofungwa na Carlos Tevez dakika ya 45.
 Carlos Tevez akimchambua kipa wa Aston Villa, kabla ya kuifungia timu yake bao pekee
 Kiungo Jack Rodwell akiugulia maumivu katika mechi hiyo. Rodwell atakuwa nje kwa muda kutokana na kuumia huko
 Wachezaji wa Man City wakimpongeza Tevez baada ya kuifungia bao pekee dhidi ya Aston Villa.
Mshambuliaji Christian Benteke wa Aston Villa, akifumua shuti langoni kwa Manchester City, wakati wa mechi ya Ligi Kuu ya Uingereza baina ya timu hizo iliyofanyika jana Jumatatu usiku kwenye Uwanja wa Villa Park, ambapo Man City ilishinda bao 1-0 lililofungwa na Carlos Tevez.
Winga David Silva wa Manchester City (kushoto), akitafuta mbinu za kumtoka Fabian Delph wa Aston Villa, wakati wa mechi ya Ligi Kuu ya Uingereza baina ya timu hizo iliyofanyika Jumatatu usiku kwenye Uwanja wa Villa Park, ambapo Man City ilishinda bao 1-0 lililofungwa na Carlos Tevez.
Kiungo wa Mancester City, Yaya Toure (kushoto) akichuana na mchezaji wa Aston Villa, wakati wa mechi ya Ligi Kuu ya Uingereza baina ya timu hizo iliyofanyika Jumatatu usiku kwenye Uwanja wa Villa Park, ambapo Man City ilishinda bao 1-0 lililofungwa na Carlos Tevez.

No comments:

Post a Comment

Pages