ACAPULCO,
Mexico
NYOTA wa tenisi duniani, Rafael Nadal (pichani kulia) amemchapa Mhispania
mwenzake Nicolas Almagro kwa seti mfululizo za 7-5 6-4 na kufuzu fainali ya michuano ya Mexican Open
3013.
Nadal, ambaye hivi karibuni alirejea viwanjani akitoka
kuuguza majeraha ya miezi saba aliyokuwa akikabiliana nayo, sasa atacheza
fainali na bingwa mtetezi wa michuano hii David Ferrer pia wa Hispania.
Mkali huyo ambaye ni bingwa mara 11 wa Grand Slam, alimaliza
nafasi ya pili katika michuano ya Chile Open, kabla ya kuibuka bingwa wa Brazil
Open wiki mbili zilizopita.
Nadal sasa anatarajia kupigana kuwania ubingwa wake wa 38 wa
kwenye viwanja vya udongo kwa kumuumana na mpinzani wake Ferrer, ambaye
ameshinda mechi 19 mfululizo katika michuano hii hapa Acapulco na sasa anasaka
taji la tatu mwaka huu.
Kwa upande wake Ferrer, alifanya kazi ya ziada kuibuka
mshindi na kutinga fainali kwa kumchapa Mtaliano Fabio Fognini kwa 6-3 6-7 (5)
6-1, katiika pambano lililodumu kwa masaa mawili na dakika 23.
Fainali ya Nadal na Ferrer inatarajiwa kupigwa leo Jumapili,
huku kila mmoja akipewa nafasi sawa na mwingine kuweza kuibuka mbabe wa michuano
hii.
BBC
No comments:
Post a Comment