MANCHESTER,
England
BAADA ya kufanikiwa kurefusha kwa miezi 12 mkataba wa Ryan
Giggs, kocha wa Manchester United, Sir Alex Ferguson – sasa amegeukia kwa beki
wa kati wa klabu hiyo, Rio Ferdinand ili naye asaini nyongeza ya msimu mmoja.
Giggs, jana alitarajiwa kuingia katiika dimba la Old
Trafford kucheza mechi yake ya 1,000 akiwa na Man United, tangu alipoichezea
mechi yake ya kwanza miaka 22 iliyopita.
Ferguson
alisema jana kuwa, anatarajia kumuona Ferdinand, 34, akirefusha zama zake klabuni
Old Trafford anakomaliza muda wake wa mkataba kiangazi hiki.
Bosi huyo wa United alisema: “Itakuwa uwezekano wenye nguvu
kuu. Nadhani alifanya mengi makubwa na ya kuvutia msimu uliopita. Alijiongoza
yeye binafsi katika njia sahihi.”
Aidha, Fergie, alienda mbali na kuzungumzia kiwango na
maisha ya Giggs dimbani tangu kutua kwake mikononi mwake: “Kipi nitasema kuhusu
Giggs ambacho bado sijawahi kusema?
“Ni mchezaji wa kustaajabisha, wa kipekee kwa kila mtu. Ryan
ni mfano wa kuigwa kwa sisi sote. Kiwango chake alichoonesha mwaka huu na
furaha yake ya mchezo, imeonesha ni kwa namna gani alikuwa na kila sababu ya
kurefusha uwepo wake hapa.”
Kwa upande wake, Giggs alisema: “Najisikia vizuri, nafurahia
soka langu kuliko kipindi chochote maishani na, kitu muhimu, najihisi kuwa na
mchango mkubwa kwa timu.”
The Sun
No comments:
Post a Comment