Winga Teleza Kazini: Theo Walcott wa Arsenal katikati, akipangua mabeki wa Everton katika mechi ya Ligi Kuu kwenye Uwanja wa Emirates jijini London jana usiku, iliyoisha kwa wenyeji Gunners kubanwa mbavu na kutoka sare tasa ya 0-0.
Kama Vitani Vile!! Kiungo Jack Wilshere wa Arsenal, akipiga mweleka wakati wa mchuano wake na mchezaji wa Everton, katika mechi ya Ligi Kuu usiku wa kuamkia leo kwenye dimba la Emirates.
Mpira Uende, We Ubaki: Kiungo wa Everton, Fellaini kulia akichuana na nyota wa Gunners katika mechi hiyo.
Mchuano Mkali Dimbani: Haikuwa rahisi kwa timu hizo, vita ilikuwa kali baina ya wachezaji wa kila timu, huku kila mmoja akitaka kuonesha umahiri wake kama inavyoonekana hapa.
Mtu Kati!!! Walcott akikabwa na wachezaji wa Everton katika staili ya 'mtu kati' wakati wa mechi hiyo.
Siamini Macho Yangu! Nyota wa Gunners, akiwa aamini kama jaribio lake la kutikisa nyavui limeokolewa na kipa wa Everton ambaye anapongezana na mchezaji mwenzake kwa nyuma kama wanavyoonekana.
Hutanitambua: Jack Wilshere wa Gunners, akikabwa koo na Kevin Mirallas wa Everton wakati wa mechi hiyo.
Si Ulijifanya Mbabe Uwanjani? Jack Wilshere akilipiza kumkaba shingo mchezaji Kevin Mirallas wa Everton wakati timu zilizpokuwa zikiingia vyumbani wakati wa mapumziko.
Mpaka Kieleweke: Vita ya Wilshere na Mirallas, iliendelea hata baada ya filimbi ya mwisho katika njia ya kuingilia vyumba vya kuvalia. Pichani wachezaji hao wakitenganishwa na wenzao.
No comments:
Post a Comment