HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

April 15, 2013

Benki ya Exim yazindua tawi la tatu Comoro


 Rais wa Comoros Dr. Ikililou Dhoinine, akikata utepe kuzindua tawi la tatu la Benki Exim nchini humo katika hafla fupi iliyofanyika mwishoni mwa wiki. Kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya Exim Yogesh Manek. (Na Mpiga Picha Wetu)
Rais wa Comoros Dr. Ikililou Dhoinine akisaini kitabu cha wateja wakati wa hafla ya uzinduzi wa tawi la tatu la benki ya Exim mwishoni mwa mwaka. Wapili kulia ni Mkurugenzi mtendaji wa Banki ya Exim Tanzania Anthony Grant na Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya Exim Yogesh Manek.

FOMBONI, COMORO

BENKI ya Exim ya Tanzania imeendelea kijiimarisha nchini Comoro baaada ya kuzindua tawi lake la tatu katika mji wa Fomboni ambalo litasaidia kuongezaka kwa upatikanaji wa hudumas za kibenki nchini humo.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa tawi hilo mwishoni mwa wiki, Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya Exim, Yogesh Manek alisema kuwa tawi hilo jipya litasaidia kuchangia kikamilifu maendeleo ya sekta ya kifedha nchini humo ikiwa ni kutekeleza dhamira ya kupeleke huduma za kibenki karibu na jamii mbali mbali.

“Miaka mitano iliyopita, nilifungua tawi la kwanza la Benki ya Exim hapa Comoro. Ninafuraha kushiriki tena katika uzinduzi wa tawi letu la tatu la Mohelli hapa Comoro leo hii.

“Uzinduzi wa tawi hili jipya unadhihirisha muendelezo wa jitihada za benki yetu  katika kuchangia maendeleo ya kifedha na kiuchumi katika nchi ambazo benki yetu inatoa huduma.

 “Benki ya Exim itaendelea kufanya kazi ikilenga kuweka uwiano baina ya faida inayopata na utohaji wa huduma bora na za kipekee kwa wateja wetu ,” alisema Bw. Manek.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Exim, Anthony Grant wakati wa hafla hiyo alisema kuwa dhamira kuu ya benki yake kama taasisi ya fedha ni kuzidi kutanua huduma zaidi nchini Comoro hususani kwenye sehemu ambazo bado hazijafikiwa na taasisi yoyote ya Kifedha.

“Nachukua nafasi hii kuwahakikishia kuwa Benki ya Exim itaendelea kuwepo hapa na tutafanya kila jitihada kuhakikisha biashara mpya na zilizopo sasa nchini Comoro ,” alisema Grant.
Kwa upande wake, Gavana wa Benki Kuu ya Comoro, Mohamed Ali alisema kuwa uzinduzi wa tawi hilo jipya la Benki ya Exim utakuwa chachu ya maendeleo ya sekta ya kibenki nchini humo.
Hafla hiyo ilihuidhuliwa na viongozi mbali mabali nchini Comoros pamoja na raisi wa nchi hiyo Dr. Ikililou Dhoinine.

No comments:

Post a Comment

Pages