HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

April 03, 2013

BOB JUNIOR AIBUKA NA 'KIZEMBE'


Na Elizabeth John

“Namshukuru mungu nimerejea salama, naomba mashabiki wangu wakae mkao wa kula kwaajili ya kuipokea kazi hii ambayo tayari imeanza kufanya vizuri katika vituo mbalimbali vya redio"

MTAYARISHAJI na msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini, Rahim Rummy ‘Bob Junior’ ameachia ngoma yake mpya inayokwenda kwa jina la ‘Kizembe’ ambayo imeana kufanya vizuri katika vituo mbalimbali vya redio.

Kabla kuachia kazi hiyo, Bob Junior alikua anatamba na kibao chake cha ‘Nichuum’ ambacho kinafanya vizuri katika vituo mbalimbali vya redio.

Akizungumzia kazi hiyo, mkali huyo alisema ameitengeneza nchini Poland ambapo alikua ameenda kwa ajili ya mapumziko ya siku kadhaa.

“Namshukuru mungu nimerejea salama, naomba mashabiki wangu wakae mkao wa kula kwaajili ya kuipokea kazi hii ambayo tayari imeanza kufanya vizuri katika vituo mbalimbali vya redio".

Alisema kwasasa yupo katika maandalizi ya kutengeneza video ya kazi hiyo ambayo anatarajia kuiachia hivi karibuni.

No comments:

Post a Comment

Pages