Na Bryceson Mathias
'Si vizuri kunyamaza kimya; hasa hali inapoliendea Bunge vibaya'
SIJUI Wabunge nani kawaroga na sielewi mnajisikiaje, maana hamuoni kuwa nchini kuna watu wanalalia mizizi, matunda ya porini, uji wa chumvi na wengine mulo mmoja kwa siku, huku ninyi mnashiba kwa siagi na chakula hadi kinamwagwa, matokeo yake mnatukana badala kusuguaa vichwa.
Nnilitegemea wabunge Mtasugua vichwa ili kusumbukia maisha ya wananchi hasa wanyonge wasio na kitu, walale wapi, wavae nini, wale nini, wanywe nini; yu mkini miili yao iwe na afya waishi maisha marefu, lakini sivyo mnavyofanya.
Biblia Yeremiea 9:17-19 inasema” Fikirini ninyi, mkawaite wanawake waombolezao, ili waje; mkatume na kuwaita wanawake wenye ustadi, ili waje; na wafanye haraka na kutuombolezea, ili macho yetu yachuruzike machozi, na kope zetu zibubujike maji.
Wabunge tumewatuma mkatuombolezee serikalini kwamba, hali, nchi imetekwa na mafisadi, na wawekezaji uchwara, twiga wetu wenye gharama za mamilioni, wanaingizwa kwenye ndege wazima wazima na maisha wananchi ni ngumu, wanalala na njaa. Ninyi mnatukana!.
Badala ya kupigania Viwanda vilivyoporwa na kuawa kama Tanganyika Pakers, Viwanda vya Nguo, Viwanda vya Viatu, virejeshwe toka kwa mafisadi wananchi wauze mali ghafi halisi (mazao yao) ili wawe na chakula kizuri, Mavazi ,mahali pa kulala na afya nzuri, ninyi mnakuwa watumwa wa kutangaza itikadi na kukuza majina ya watu! Ni aibu!!
Tulitegemea Biblia inavyosema, Nina watu nimejisazia huko wanaolicha Neno langu, mbona mumo humo mmekuwa Bubu, mmefumba vinywa vyenyu? Asante kwa wale wenye Mimba ya utungu wa watanzania, si kwamba hatuwaoni tunawaona! Mungu atawalipa. “sasa tumeng;amua kwa mlitaka Bunge lisioneshwe”
Mlijisahau nawakumbusha; “Angalia, utakapokuwa umekula na kushiba, na kujenga nyumba nzuri na kukaa ndani yake; na makundi yako ya ng'ombe na kondoo yatakapoongezeka, na fedha yako na dhahabu yako itakapoongezeka, na kila kitu ulicho nacho kitakapoongezeka; basi hapo moyo wako usiinuke, ukamsahau Bwana, Mungu wako, aliyekutoa katika nchi ya Misri, katika nyumba ya utumwa Kumb. 8:12-14.
Baada ya kuwachagua, mmepata Mashangingi, Nyumba mnakula vizuri, mna posho nzuri kila kikao, mnawaona wapiga kura hawafai, hamtaki mawazo yao, hamwatetei, ila kwenda na mawazo yenu ya kuwashukuru wake zenu na watoto wenu kila mnapoinuka. Je waliwachagua peke yao?.
Wabunge; nawaonya Bwana Mungu asema hivi. “ Mwenye kudhulumu na azidi kudhulumu; na mwenye uchafu na azidi kuwa mchafu; na mwenye haki na azidi kufanya haki; na mtakatifu na azidi kutakaswa. Tazama, naja upesi, na ujira wangu u pamoja nami, kumlipa kila mtu kama kazi yake ilivyo.
Mungu anasema; “Mimi ni Alfa na Omega, mwanzo na mwisho, wa kwanza na wa mwisho. Heri wazifuao nguo zao, wawe na amri kuuendea huo mti wa uzima, na kuingia mjini kwa milango yake. Huko nje wako mbwa, na wachawi, na wazinzi, na wauaji, na hao waabuduo sanamu, na kila mtu apendaye uongo na kuufanya ufunuo.22:11-15
Nataka wabunge mjitakase kama Makuhani nao, walivyomkaribiao Mungu, wakajitakasa, ili Bwana asije akawafurikia. anapoona watu wake wanateseka kwa shida na maisha magumu ya bei za vitu, usafiri vikipanda bila kukemewa.
0715-933308



No comments:
Post a Comment