HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

April 24, 2013

Chadema Kushambulia Jimbo la Kongwa


Na Bryceson Mathias,Kongwa
WABUNGE watano wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) walitiomuliwa bungeni na kuamriwa kukaa nje ya Bunge kwa siku tano kutokana na vurugu zilizotokea hivi karibuni, wanatarajiwa kushambulia Jimbo la Kongwa katika Kata Tano.
Wabunge hao wanaotarajiwa ni pamoja na Mnadhimu Mkuu wa Upinzani, Tundu Lissu (Singida Mashariki) , Hezekiah Wenje (Nyamagana), Highness Kiwia (Ilemela), Joseph Mbilinyi (Mbeya Mjini) Godbless Lema (Arusha Mjini) na Mchungaji Peter Msigwa (Iringa Mjini).
Akizungumza na Tanzania Daima jana Mwenyekiti wa Chadema Wilaya ya Kongwa, Juma Chibiriti amesema, hakubaliani na Kitendo cha Wabunge wa Chadema kufukuzwa, ila makosa  aliyofanya Naibu Spika kwa wabunge hao, akidai uwepo wao jimboni humo unatarajia kuwapa Wanachama 300 kwa M4C.
“Wabunge wetu asubuhi watashambulia Kata za Ngomai, Njoge (Hembahemba), Pandambili, Mlali (Bondeni) na Majumuisho yatafanyika Mji Mdogo wa Kibaigwa”.alisema Chibiriti akijiamini kuwa mikutano hiyo itateka hisia za Wananchi.
Aidha Chibiriti aliongeza kuwa, uongozi wa Chadema Wilaya bado unauomba Uongozi wa Chadema Taifa, kuwaongezea Nguvu kwa kumuongezea Mbunge Machachari John Mnyika ili aungana na wenzake ili kuongeza mashambulizi ya M4C zaidi ya Kata Tano, iwapo itawezekana.
Awali mapema Uongozi wa Bunge awali ulisema, Chanzo za kufukuzwa kwa Wabunge hao ulikuwa ni kuwazuia askari wa Bunge kumtoa nje Lissu ambaye alikuwa ameamriwa kutoka nje na Naibu Spika, Job Ndugai baada ya kuingilia hotuba ya Mbunge wa Iramba Mashariki, Mwigulu Nchemba
 

No comments:

Post a Comment

Pages