David Luiz wa Chelsea akishangilia na wenzake bao lililowapa ushindi wa 2-1 dhidi ya FC Basel ya Uswisi katika katika mechi ya kwanza ya nusu fainali ya Kombe la Europa League kwenye Uwanja wa St Jaco-Park jana usiku.
Nyota wa Basel Marco Streller akisikitika baada ya kupoteza nafasi muhimu kuifungia timu yake bao dhidi ya Chelsea.
Fabian Schar wa Basel akishangilia baada ya kuifungia timu yake bao la kusawazisha kwa mkwaju wa penati
Fabian Schar akipiga penati hiyo.
Beki wa Basel akilala kumzuia Eden Hazard wa Chelsea, huku Fernando Torres akiwa tayari kutoa msaada.
Kocha wa Chelsea Rafa Benitez akimpa mpira wa kurusaha nyota wake Victor Moses ambaye alifunga bao la kwanza la Blues kunako dakika ya 12.
Picha mbili za juu na chini zinamuonesha Moses akishangilia kwa kuruka sarakasi baada ya kuifungia Chelsea bao la kuongoza.
Moses (13) akiuangalia mpira wake wa kichwa ukitinga nyavuni kuiandikikia Chelsea bao la kwanza.
Beki wa Basel (14) akimchezea rafu yoso Cesar Azpilicueta wa Chelsea, rafu ambayo ilionekana wazi kuwa ni penati, ingawa mwamuzi hakutoa maamuzi hayo na kuzua malalamiko kwa Benitez.
David Luiz akimkanyaga nyota wa Basel Phillip Degen. Ingawa refa hakuiona rafuu ipasavyo, kuna kila dalili Luiz akafungiwa mechi moja na Kamati husika itakayomlazimu akose mechi ya marudiano.
David Luiz akipiga adhabu ndogo 'free kick' iliyozaa bao la ushindi la Chelsea.
BASEL, Uswisi
Katika nusu fainali nyingine, Fernabahce ya Uturuki ikiwa
nyumbani Sukru Saracoglu, iliibuka na ushindi mwembamba wa bao 1-0 dhidi ya
Benfica ya Ureno, ambapo washindi wa mechi hizo wataumana fainali huko
Amsterdam Arena, Mei 15
CHELSEA wamenusa fainali ya michuano ya pili kwa ukubwa
ngazi ya klabu barani Ulaya ‘Europa League’ baada ya jana usiku kuichapa FC Basel ya hapa
kwa mabao 2-1 na kujiwekea mazingira mazuri kuelekea mechi ya mrudiano.
Ikicheza ugenini katika dimba la St Jacob-Park juzi usiku,
Chelsea ilitangulia kufunga mapema dakika ya 12 ya mpambano huo, shukrani kwa
bao la Mnigeria Victor Moses.
Ni bao lililoonekana kutaka kuitoa dimbani na ushindi, kabla
ya Fabian Schar kufunga kwa penati tatatishi dakika tatu kabla ya filimbi ya
mwisho kuisawazishia Basel iliyokuwa ikishangiliwa mno na mashabiki wake.
Wakati kila mmoja akiamini pambano linaisha kwa sare ya bao
1-1, katika dakika za nyongeza David Luiz aliifungia Chelsea bao maridadi la
‘mpira uliokufa’ kuipa ushindi muhimu kuelekea marudiano ya Alhamisi ijayo
kwenye dimba la Stamford Bridge.
Kocha wa Chelsea, Rafa Benitez alisema kuwa ‘alishangazwa
mno’ na mwamuzi Pavel Kralovec kuinyima timu yake penati, baada ya Valentin
Stocker kumchezea rafu yoso Cesar Azpilicueta, na kwamba bao la ‘usiku’ ni
malipizi ya dhuluma ya mwamuzi huyo.
Benitez akaenda mbali kwa kuwataka nyota wake kutobweteka na
ushindi huo, badala yake wajipange ipasavyo kuwakabili wapinzani wao hao katika
mechi ya marudiano Mei 2 wiki ijayo na kujikatia tiketi ya michuano hiyo.
"Tulipaswa kufanya jambo kutoruhusu bao lao, ambalo
lilikuwa ni zaidi ya motisha kwao mchezoni.
"Mlinda mlango wao pia angekuwa na uwezo wa kuzuia mpira
wetu wa adhabu ndogo ‘free-kick’, lakini mwisho wa siku tulifunga bao ambalo
kila mmoja nadhani anajua kwamba lilikuwa la haki."
Katika nusu fainali nyingine, Fernabahce ya Uturuki ikiwa
nyumbani Sukru Saracoglu, iliibuka na ushindi mwembamba wa bao 1-0 dhidi ya
Benfica ya Ureno, ambapo washindi wa mechi hizo wataumana fainali huko
Amsterdam Arena, Mei 15.
Supersport.com
No comments:
Post a Comment