Kikosi cha timu ya Benki ya Exim kikiwa katika picha ya
pamoja kabla ya mchezo wa kirafiki dhidi ya Benki ya KCB uliofanyika kwenye
Uwanja wa Don Bosco jijini Dar es Salaam juzi. Exim ilishinda kwa mabao 4-3.
(Na Mpiga Picha Wetu)
Na Francis Dande
TIMU ya soka ya Benki ya Exim
(Innovation FC) imezidi kudhihirisha umahiri wake dimbani baada ya juzi
kushinda mabao 4-3 dhidi ya KCB FC katika mechi ya kirafiki iliyochezwa kwenye
viwanja vya Don Bosco, jijini Dar es
Salaam .
Ikicheza soka maridadi, hadi
mapumziko vijana wa Exim FC walikuwa mbele kwa mabao mawili yakiwekwa wavuni na
Ally Sumar dakika ya 15 kabla ya Norbert Misana kufunga la pili dakika ya 41.
Katika kip;indi hicho cha
kwanza, licha ya KCB FC kuonesha kiwango cha kuvutia, lakini walishindwa kupata
bao kutokana na mbinu kali za ukuta wa wapinzani wao.
Kipindi cha pili kilianza kwa
KCB FC kucheza kwa juhudi kubwa na kufanikiwa kusawazisha mabao hayo katika
dakika za 50 na 60, yote yakifungwa na nyota wake hatari, Raymond Bunyinyig.
Hata hivyo, dakika ya 64, Exim
FC walirejea mchezoni na kupata bao la tatu likifungwa na
Stephen Kimei, lakini KCB FC
nao walizinduka na kusawazisha bao mhilo dakika ya 76.
Matokeo hayo yakaongeza kasi ya
mchezo kwa kila timu kusaka bao la ushindi na katika dakika ya 85, ndipo Exim
FC walipata bao la nne, likifungwa na
Lusajo Adam.
Akizungumza baada ya mechi
hiyo, naodha wa Exim FC, Fadhili Seleman aliwapongeza wachezaji wa timu hiyo na
kusema ushindi huo ulitokana na juhudi za kila mchezaji dimbani.
Alisema ufanisi wa timu hiyo ni
kutokana na sapoti wanayopata kwa uongozi wa benki hiyo kwa kutambua umhimu wa
michezo katika maisha ya
kila siku.
Fadhili ameongeza kuwa kwa
mazingira hayo, anaamini timu hiyo itaendelea kufanya vizuri dhidi ya timu
nyingine zinazomilikiwa na benki hapa nchini.
No comments:
Post a Comment