Mkurugenzi Mkuu wa Kuku Foods (Kampuni tanzu ya
KFC), Nic Melt-Bey akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo wakati wa uzinduzi wa tawi la Mikocheni jirani na shule ya FEZA.
Mwanachama wa Kuku Foods, Faraja Kihongole akifafanua jambo wakati wa uzinduzi wa tawi jipya la Kampuni tanzu ya KFC jijini Dar es Salaam leo.
Wanachama wa Kuku Foods wakiimba wakisherehekea uzinduzi huo kwa kuimba nyimbo.
Mhariri wa Habari Mseto Blog, Salum Mkandemba akipata msosi wakati wa uzinduzi huo.
Faraja Kihongole na Jackline
Wanachama wa KFC
Faraja Kihongole na Jackline
Wanachama wa KFC
Na Mwandishi Wetu
KAMPUNI ya KFC inayojihusisha na uuzaji wa vyakula
(migahawa) katika mataifa mbalimbali duniani, leo imefungua tawi jipya
Mikocheni, jijini Dar es Salaam, huku ikiwa katika harakati za mwisho za
kufungua tawi la pili Septemba mwaka huu.
Akizungumza katika uzinduzi huo, Mkurugenzi Mkuu wa Kuku
Foods (Kampuni tanzu ya KFC), Nic Melt-Bey, alisema, KFC inayofuraha
kuiunganisha Tanzania na mataifa mengine ya Afrika na Dunia, katika kupewa
huduma bora na za kisasa za vyakula.
Alisema kuwa, mchakato uliowezesha ufunguzi wa tawi jipya la
Mikocheni, umedumu kwa muda wa miaka mitatu, ukifanyia tathmini masuala
mbalimbali, ikiwamo mafunzo kwa wahudumu, ili kuwaboreshea uwezo katika kuhudumia
sekta ya vyakula.
“KFC inasubiri kwa hamu kuona namna Watanzania
watakavyotumia fursa ya uwapo wa matawi yetu nchini, katika kujipatia huduma
bora, za kisasa na za haraka. Furaha yetu pia ni kuanza kuhudumia soko la
Tanzania, ikihusisha vyakula vya ndani na nje ya nchi,” alisema Melt-Bey.
Alisema kuwa, KFC imejikita katika utoaji wa huduma za
vyakula duniani kote na ina migahawa zaidi ya 17,000 na kwamba Septemba mwaka
huu itafungua tawi la pili jijini Dar es Salaam, katika jengo la Diamond Plaza.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Biashara wa Kuku Foods, Simon
Schaffer, aliwahakikishia wakazi wa Dar es Salaam kuwa, zama zao za kupata
huduma bora za vyakula kama zitolewazo katika migahawa mingine ya KFC duniani
kote, zimewadia.
No comments:
Post a Comment