HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

May 01, 2013

DORTMUND HIYOOO FAINALI ULAYA LICHA YA KUDUNDWA 2-0 NA MADRID

Mshambuliaji Karim Benzema akishangilia bao la pili la Real Madrid na lililofungwa na Sergio Ramos (kulia) na kuifanya Madrid kushinda kwa mabao 2-0 dhidi ya Borussia Dortmund ya Ujerumani katika mechi ya marudiano nusu fainali. Katika mechi ya kwanza Jumatano iliyopita huko Signal Iduna Park, Dortmund ilishinda 4-1, hivyo Wajerumani hao jana wamefuzu fainali kwa ushindi wa jumla wa mabao 4-3.
 Sergio Ramos akipiga shuti kufunga bao la pili la Madrid dakika ya 87 katika mechi hiyo kwenye Uwanja wa Santiago Bernabeu jijini Madrid, ambapo wenyeji walishinda mechi kwa mabao 2-0, ingawa hayakutosha kuwapeleka fainali Wembley.
 Benzema hapo akifunga bao lake katika dakika ya 81 kuipa uongozi muhimu Madrid.
 Wachezaji wa Madrid, wakimnyang'anya mpira mlinda mlango wa Dortmund, Roman Weidenfeller aliyeonekana kama kupoteza muda kujaribu kupunguza kasi ya wenyeji waliokuwa wakisaka bao la ushindi ili kufuzu fainali ya mabingwa Ulaya.
 Mshambuliaji wa Madrid, Cristiano Ronaldo (ambaye hakufunga jana), akimiliki mpira huku akiwa amezungukwa wachezaji wanne wa Dortmund katiika mtanange huo.
 Mtikisa nyavu wa Dortmund, Robert Lewandowski, akiungalia mpira wake aliojaribu kufunga ukitoka sentimita chache huku kipa wa Madrid na beki wake pia wakiukodolea macho mpira huo.
 Mshambuliaji wa Madrid, Gonzalo Higuain akijaribu kupokonya mpira mikononi mwa kipa wa Dortmund, Weidenfeller, huku beki wake Mats Hummels akitoa msaada wa kumbana Higuain.
 Lewandowski akiruka juu kuwania mpira na yoso Raphael Varane wa Madrid.
 Ronaldo akilalamikia rafu aliyofanyiwa, kama ilivyo kwa kocha wake Jose Mourinho (chini) ambaye alikuwa akipinga maamuzi ya refa Howard Webb wa England.

Ronaldo aakiondoka uwanjani kwa huzuni, baada ya mabao mawili ya kikosi chake kushindwa kuwabeba na kuwafikisha fainali ya mabingwa Ulaya.

No comments:

Post a Comment

Pages