Na Elizabeth John
MKALI wa
muziki wa kizazi kipya nchini, Moses Bushagama ‘Mez B’ ameachia kibao chake
kipya kinachokwenda kwa jina la ‘Kidela’ ambacho kimeanza kufanya vizuri katika
vituo mbalimbali vya redio.
Mez B alishawahi kutamba na kibao chake cha
‘Kama vipi’ alichoimba na mwanadada Rehema Chalamila ‘Ray C’ ambacho kilifanya
vizuri zaidi mbali na kuwa na vibao vingi ambavyo vilitamba kipindi hicho.
Akizungumzia kazi hiyo mkali huyo alisema aliifanya
na marehemu Sharo Milionea lakini kutokana na sababu ambazo zilikuwa nje ya
uwezo wao walishindwa kuitoa kwa wakati na kulazimika kuitoa kipindi hiki.
“Kazi hii niliifanya na mkali wa muziki huo
marehemu Sharo lakini kuna vitu viliingiliana tukashindwa kuachia kwa wakati,
lakini baada ya kufariki kwa msanii huyo nilishindwa kuitoa nikaona nitafute
mtu mwingine badala yake,” alisema Mez B.
Mez B alisema kwasasa yupo katika maandalizi ya
kufanya video ya wimbo huo ambayo anaifanyia katika studio ya Smart Music chini
ya mtayarishaji wake Mbezi, iliyopo Tabata jijini Dar es Salaam.
Pia aliwataka mashabiki wake kukaa mkao wa kula
kwaajili ya kuipokea kazi hiyo ambayo ipo katika hatua za mwisho za uandaaji
ikiwa ni pamoja na kazi nyingine ambazo zinafuata.
No comments:
Post a Comment