HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

April 07, 2013

LIGI YA DARAJA LA TATU NGAZI YA MKOA – MARA YALALAMIKIWA

Ø Tunaandika kwako malalamiko yetu moja kwa moja kuja kwako kwa sababu hatuna imani na chama cha mkoa na kamati ya ligi.

Ø Tulikaa kikao timu husika, Chama mkoa, kamati ya ligi, tukaamua kuwa ligi ianze kikanda kufuatana na Jiografia ya mkoa wetu, kituo kimoja kiwe na timu za Wilaya ya Tarime, Rorya, na Serengeti, na kituo kingine timu za Wilaya Musoma Mjini, Musoma Vijijini na Bunda, na ligi hiyo itakuwa ni ya nyumbani na ugenini kama maelekezo ya TFF yalivyoelekeza kwenye waraka wake kwa vyama vya soka vya mikoa, tukaondoka na maazimio hayo.

Ø Chakushangaza tulipata ratiba isiyokuwa na kanuni yenye maelekezo kinyume na maazimio yetu kwenye kikao,kuwa ligi itakuwa kwenye kituo kimoja cha Bunda, kutakuwa na makundi mawili yenye timu nne,nne, na timu kucheza mechi tatutatu na kila kundi litatoa timu mbili zitakazocheza kupata bigwa wa mkoa, hapo hapo kwenye kituo cha bunda. 

Hivyo hakuna nyumbani na ugenini, kitu ambacho timu zinazotokea nje ya Bunda zinaingia gharamakubwa huku timu za Bunda zikinufaika na mfumo huo kwani wao mechi zote wako nyumbani kwa namna moja huu ni uonevu kwa timu zinazotoka wilaya nyingine tofauti na Bunda. Kwa maana hiyo maelekezo ya TFF tayari hayakufuatwa kuwa ligi ichezwe kwa mtindo wa nyumbani na ugenini huu ni ukiukwaji wa kanuni.

Ø Vile vile makubaliano ya kikao hicho yalielekeza kuwa timu shiriki ni zile ambazo zilishiriki ligi ya mkoa kwa msimu uliopita, hazikupanda na zikabaki katika ligi hiyo. 

Cha ajabu katika timu shiriki nane zinazocheza ligi hii baadhi ya timu hazina sifa hiyo ya kushiriki katika ligi hii mfano. Polisi ya Bunda, Town star ya bunda, Musoma Shooting ,msimu uliopita hazikucheza ligi hii ya mkoa wala ligi yoyote hata daraja la nne, hatuelewi zimeingizwa kwa kigezo kipi au formula gani?!!!!

Ø Kuna baahi ya timu zinatumia wachezaji ambao wengine wamecheza ligi za msimu huu wilaya na bado wanacheza ligi ya Mkoa ndani ya msimu huu mmoja kwa maana nyingine mchezaji anacheza ligi mbili katika msimu mmoja, huu ni uvunjaji wa kanuni za ligi!!!

Ø Pamoja na yote bado waamuzi wanavunja kanuni za mpira kwa kuzipendelea timu za Bunda dhahiri bila kuchukuliwa hatua zozote kiasi cha kutufanya tuzidi kuamini huenda wanataka timu hizi ziwe mabingwa.

Ø Haitoshi ligi imeendeshwa bila ya kuwa na kanuni zozote ambazo vilabu shiriki vimegawiwa na kupata semina elekezi kama ilivyo ada. Haitoshi bado vilabu havipati hata senti moja ya mgao wa mapato ya mlangoni na hata ukiuliza hesabu zinazotumika hazieleweki.

Ø Hali kadhalika bado ratiba ya mzunguko wa pili wanaitoa siku moja kabla na kasha kuibadilisha na kuzipata taarifa vilabu siku moja kabla ya mchezo ilhali timu zimeshaingia gharama za mechi hiyo.

Ø Tunapoanadika barua yetu hii ligi inaendelea, na tumepeleka malalamiko yetu lakini hatupati majibu ya msingi. Hivyo tunaona chama, Mkoa na kamati ya ligi vinaburuza kanuni za ligi na zinalipeleka soka la Tanzania pahala pabaya.

Tunaomba muongozo na maelekezo toka juu.

AHMED FERUZI
KATIBU POLISI
0758190000 / 0655000019

No comments:

Post a Comment

Pages