Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed
Shein,akiweka shada la mauwa katika kaburi la Marehemu Rais wa kwanza wa Zanzibar Mzee Abeid Amani Karume, wakati wa
Hitma na Dua iliyoombwa na wananchi wa Zanzibar
huko Kisiwandui mjini Zanzibar jana. (Picha
na Ramadhan Othman, Ikulu)
Kiongozi wa Kanisa la Anglikana la Zanzibar akiomba dua wakati wa maadhimisho ya Siku ya Mashujaa (Karume Day) katika Makao Makuu ya CCM Kisiwandui Zanzibar leo April 7, 2013
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Rais wa Zanzibar Dkt Mohamed Ali Shein na viongozi wengine wa juu wakisoma dua wakati wa maadhimisho ya Siku ya Mashujaa (Karume Day) katika Makao Makuu ya CCM Kisiwandui Zanzibar leo April 7, 2013
Wake za vionvgozi mbalimbali pamoja na mabalozi wakiwa katika dua wakati wa maadhimisho ya Siku ya Mashujaa (Karume Day) katika Makao Makuu ya CCM Kisiwandui Zanzibar leo April 7, 2013
Kiongozi wa Kihindu akiomba dua wakati wa maadhimisho ya Siku ya Mashujaa (Karume Day) katika Makao Makuu ya CCM Kisiwandui Zanzibar leo April 7, 2013. PICHA NA IKULU.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Ali Mohamed Shein leo ameongoza hitma ya kumuombea dua Rais wa kwanza wa Zanzibar Marehemu mzee Abeid Amani Karume, iliyofanyika Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui mjini Zanzibar.
Hitma hiyo pia, ilihudhuriwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dk. Jakaya Mrisho kikwete, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Mohammed Kharib Bilal, Rais mstaafu waJamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Ali Hassan Mwinyi pamoja na Makamo wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad.
Viongozi wengine ambao walihudhuria katika hitma hiyo ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idd na Rais Mstaafu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Amani Abeid Karume, Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabhi, Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Khamis Haji, Sheikh Mussa Salum kutoka Mkoa wa Dar-es-Salaam nae pia,

alihudhuria.
Wengine ni viongozi wa serikali zote mbili na viongozi wastaafu, viongozi wa vyama vya siasa, Masheikh kutoka Zanzibar na Tanzania Bara, Wabunge na Wawakilishi, wananchui kutoka sehemu mbali mbali pamoja na Mabalozi wadogo waliopo hapa Zanzibar. Hitma hiyo ilitanguliwa na Qur-an tukufu, iliyosomwa na Ustadh Sharif Muhidin na kuongozwa na Sheikh Yussuf Mohammed Khamis.
Mara baada ya hitma hiyo, Sheikh Mkoa wa Dar-es-Salaam, Sheikh Mussa Salum alitoa mawaidha na kumuelezea marehemu mzee Abeid Amani Karume kuwa ni kiongozi aliyepigania maendeleo ya wananchi wa Zanzibar na kumuombea MwenyeziMungu ampe makaazi mema Peponi.
Akieleza kuhuhu umauti, Sheikh Mussa alisema kuwa umauti ni jambo ambalo litafika kwa kila kiumbe alichokiumba MwenyeziMungu na kusisitiza kuwa ni vizuri mwanaadamu akakumbuka asili yake na hatma
yake.
Baada ya kisomo hicho cha hitma ambacho hufanyika kila mwaka inapofika tarehe 7, Aprili, viongozi hao na wananchi waliohudhuria katika hitma hiyo walimuombea dua, marehemu mzee Abeid Karume katika kaburi lake lililopo pembezoni mwa afisi hiyo ya CCM Kisiwandui dua iliyoongozwa na viongozi wa dini tofauti akiwemo Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Omar Kabhi, Askofu Michael Hafidh kutoka Kanisa la Anglikana Zanzibar.
Viongozi na wanafamilia waliweka mashada ya maua katika kaburi la marehemu mzee Abeid Amani Karume akiwemo Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Ali Mohamed Shein, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dk. Jakaya Mrisho Kikwete, Waziri Kiongozi Mstaafu wa Zanzibar Mhe. Ramadhan Haji Faki aliyeweka shada la maua akiwakilisha wazee walioshiriki Mpinduzi ya Januari 12, 1964.
Mwakilishi wa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya Wananchi wa Tanzania Meja Jenerali Hassan Vuai Chema, Balozi Ali Karume aliyewakilisha watoto wa Marehemu Karume na Balozi mdogo wa Misri anayefanya kazi zake hapa Zanzibar Balozi Walid Mohamed Ismail aliyewawakilisha Mabalozi wenzake wa hapa nchini na Ahmed Amani Karume aliyewakilisha wajukuu.
Aidha mjane wa marehemu mzee Abeid Karume, Mama Fatma Karume, alishiriki katika hitma hiyo akiongozana na Mama Salma Kikwete, Mama Asha Balozi na Mama Pili Balozi, Mama Shadya Karume na viongozi wengine wanawake wa kitaifa wakiwemo Mawaziri, Wabunge, Wawakilishini na wananchi kutoka sehemu mbali mbali ya Zanzibar na Tanzania Bara. April 7, 1972 ndiyo siku aliyouawa Rais wa Kwanza wa Zanzibar marehemu Mzee Abeid Amani Karume na wapinga maendeleo nchini ambapo hivi leo imetimia miaka 41 tokea utokee msiba huo. Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar.

STATE HOUSE ZANZIBAR
OFFICE OF THE PRESS SECRETARY
PRESS RELEASE
Zanzibar
No comments:
Post a Comment