HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

April 30, 2013

Makinda 'amewatusi' Waandishi?


Na Bryceson Mathias
APRILI 29, 2013 akiwa Mbeya, Waziri Wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bernard Membe, alikerwa na tabia ya baadhi ya Wasomi  Wanaotumia Elimu yao kuikana Nchi yao, ambapo wamefika mahali wanaipuuza na kuonesha ubinafsi wa kuwashawishi wafadhiri wainyime misaada Tanzania.
Tabia hiyo nimeifananisha na kauli iliyotolewa na Spika wa Bunge Anne Makinda aliyoitoa bungeni akijibu mwongozo wa Mbunge wa Ubongo John Mnyika (Chadema), ambapo aliwapuuza Waandishi wa  Magezetii na vyombo vyao kuwa, hafanyi kazi na vyombo vya habari kwa  kwa sababu yanaandika habari za Uongo.
Pengine haikuwa vizuri kwa Makinda, kuvijumuisha Vyombo (Magazeti) na Waandishi wote, Iwapo Chombo kimoja au Mwandishi Mmoja aliwahi kuandika Uongo, kama ambavyo baadhi ya Wabunge kwa makusudi yao waliamua kutoa Matusi ya Nguoni bungeni, ila wandishi hawakusema Bunge limetukana.
Magazeti hayo hayo ambayo Spika anayaita yanaandika Uongo, ndiyo yaliyomnadi akiomba Ubunge, Uspikana hata sasa akiendesha Bunge yamekuwa yakiendelea kumnadi. Je, kila kinachoandikwa akiendesha Bunge, Hotuba anazotoa ndani na nje ya Bunge ni za Uongo?
Kama ni za Uongo mbona Spika Makinda, hata siku moja hajawahi kukinyoshea Chombo, Habari, na Mwandishi anayedhani aliandika Uongo ili asutwe kwa taratibu na miongozo na sheria za Kihabari, kuainisha Kero yake hiyo?
Ni wazi Makinda anafahamu vipo vyombo mahususi vya kutatua Migogoro, Malalamiko na Mafanikio ya Habari na Changamoto zake, likiwemo Baraza la Habari Tanzania (MCT), Umoja wa Vyama vya Habari Tanzania (UTPC), Vyama vya Wandishi vya Mikoa,  na Wamiliki wa Vyombo vya Habari (MOAT).
Hivyo, kimsingi kuwararua Wandishi wote bila kutenga Chombo, Mwandishi au habari husika, ni fedheha ya kuwapuuza wandishi wa nchini ambao kimsingi pamoja na mapungufu wamefanya kazi nzuri mno, kuwanandi, wabunge wenyewe akiwemo Makinda na wananchi na uchumi wao.
Kitendo hicho kimewatangza vibaya wandishi wa Tanzania Kitaifa na Kimataifa, Jambo ambalo pasipo kufahamu linaaaweza kuathiri biashara ya Magazeti na Heshima ya Wandishi kwa ujumala wao, wanapokuwa kwenye majukumu yao.
Je, Wandishi ambao wametajwa bungeni kuwa wanaandika habari za Uongo wakiwa hawapo humo, wakikusudia kugomea kuandika Shughuliza zozote atakazofanya Spika Anne Makinda na Ofisi yake, kama walivyowahi kufanyiwa Mawaziri kadhaa hadi afute Kauli, atajisikia vizuri?
Sikatai hakuna habari zinatia shaka, La Hasha! Habari hizo zipo, na wandishi wanaweza kuwa wapo, na cha ajabu unaweza kukuta vyombo vya Chama Tawala na Serikali ndiyo vinavyoongoza kupotoa habari, vikifuatiwa na vya binafsi. Je amewahi kuvinyoshea kidole?
Udhaifu kwa kila upande upo sikatai, na naamini mkulima hawezi kulima bila kujikata. Lakini ni vema kuelezana katika wema, badala ya kukurupuka na kusema maeneo kwa Jazba ambayo inabomoa murua na misingi ya mustakabali wa Kazi na Biashara tunayoitegemea.
Aidha Hata Kiti cha Spika, si kwamba maamuzi yake yote kinayofanya kwenye Kiti ni Sahihi! Mengine yanaonekana wazi kabisa pale mtu Kateleza, hadi wananchi wanaosikia wanasema Haaaaaaaaaaaaaaa kama anavyokosa mchezaji kufunga Goli!
Mfano,  pia Kiti kama wandishi kina makosa yanayotumiwa katika utaratibu unaotumika sasa wa kura za ndiyo na hapana ni wa zamani na hautendi haki, kwani huegemea zaidi uamuzi wa Spika na si wabunge. Upitishaji hoja kwa kupiga kura na “Waliosema Ndiyooo wameshinda” haufai Bungeni!
0715933308

No comments:

Post a Comment

Pages