Kwishnei: Mshambuliaji wa Man City, Carlos Tevez akimkumbatia mshambuliaji wa Man United, Wayne Rooney baada ya filimbi ya mwisho ya mechi ya mahasimu wa jiji 'Manchester Derby' iliyiopigwa jana usiku kwenye dimba la Old Trafford, ambapo City iliizabua United kwa mabao 2-1.
Sikubali: Beki na nahodha wa Man City, Vicent Kompany (aliyekaa) akizuia shuti la mshambuliaji wa Man United Wayne Rooney wakati wa mechi baina yao iliyopigwa usiku wa kuamkia leo huko Old Trafford.
Hongera: Serigio 'Kun' Aguero wa Man City akishangilia bao lake dhidi ya Man United.
Maskini Weeee!!!! Vicent Kompany (kushoto) wa Man City, akipiga ndivyo sivyo kichwa na kujifunga bao, alipojaribu kuzuia kichwa na Phill Jones wa Man United (katikati juu).
Kitu kambani: Beki wa Man United, Phil Jones (4), akishuhudia kichwa cha Serrgio Aguero kikitinga nyavuni kuipa Man City bao la ushindi.
Tulia dogo: Beki Rio Ferdinand wa Man United (kulia) akimtuliza kiungo Gareth Barry (katikati) aliyekuwa akilalamikia mchezo mbaya wa mkongwe huyo wakati wa mechi ya mahasimu jana usiku.
Si umeambiwa tulia? Winga wa United, Ryan Giggs akimualia Gareth Barry aliyekerwa na rafu za Rio Ferdinand katika mechi hiyo.
Hureeeeee!!!! Phil Jones wa Man United akishangilia bao la kusawazisha
Nafunga hivi!!!! Kiungo James Milner wa Man City (7), akiifungia timu yake bao la uongozi katika mechi hiyo ya Ligi Kuu.
Tumekuja kuwashika: Wachezaji wa Man City wakimpongeza mwenzao James Milner (7), baada ya kuifungia tyimu yake bao la kwanza.
Nimewafyeka hivi: Kiungo James Milner akishangilia kwa staili ya mchezo wa gofu (kufyeka), baada ya kufunga bao la kwanza la Man City dhidi ya Man United.
Unyama unyamani: Beki Phil Jones wa Man United kushoto, akichuana kuhakikisha Carlos Tevez hafungi bao katika shambulizi hili.
Hawa jamaa noma aisee!!! Wachezaji wa Man United, Wayne Rooney, Michael Carrick na Robin van Persie wakiwa hawaamini macho yao baada ya kuchapwa bao na Man City. Hapa walikuwa wakisubiri kipyenga ili kuanza mchezo.
Hakuna bao: Carlos Tevez akijaribu bila mafanikio kufunga bao kutokea 'engo' ngumu huku akichungwa na Rio Ferdinand na kipa David de Gea wa Man United.
Jaribio la mapema: Mholanzi Robin van Persie wa Man United (katikati) akipiga shuti kujaribu kufunga mapema baada ya kuanza kwa mpambano huo.
Mpira uende, we ubaki: Van Persie akimtoka Kompany
Malalamiko kwa mwamuzi: Pablo Zabaleta wa Man City akimlalamikia mwamuzi Mike Dean, baada ya kupuliza kipenga cha mapumziko 'katikati ya sherehe'.
Kona kichovu: Mshambuliaji Wayne Rooney akiwa ameshika mpira kwenda kupiga kona akiwa amechoka.
Malalamiko kwa refa: Kocha wa Man City, Roberto Mancini kulia, akimlalamikia mwamuzi Mike Dean.
Beki hasifiwi bana!!! Nahodha wa Man United, Patrice Evra, akiganda mabegani mwa James Milner na kupiga kichwa kuondosha hatari langoni kwake.
Mabosi dimbani: Watoto wa mmiliki wa Man United Malcom Grazer, Joel Grazer (kulia), Avram Grazer (katikati), wakiwa wanafuatilia mtanange huo na David Gill.
Mserbia benchi: Nemanja Vidic wa Man United akiwa benchi
Mimi noma mzee!!! Mtaliano anayeinoa Man City, Roberto Mancini, akimpa mkono Mskochi wa Man United, Sir Alex Ferguson baada ya filimbi ya mwisho ya mtanange huo.
Usitukane mamba kabla hujavuka mto: Mashabiki wa klabu ya Man United, wakionesha bango lililoandikwa 'Our players make history, your players make money' (Wachezaji wetu wanaandika historia, wachezaji wako wanakusanya pesa). Bango hili lilikuwa likiwabeza nyota wa City kuwa wako kipesa zaidi, huku wale wa United wakiwa kimafanikio zaidi. (Picha zote kwa hisani ya gazeti la Daily Mail la Uingereza)
No comments:
Post a Comment