HABARI MSETO (HEADER)


April 09, 2013

MABINGWA ULAYA: GALATASARAY, MADRID VITANI (TTA) LEO


Mshambuliaji Cristiano Ronaldo wa Real Madrid (katikati) akifunga bao wakati wa Mechi ya kwanza kati ya timu yake na Galatasaray, ambazo leo zinarudiana kwenye Uwanja wa Turk Telecom Arena (TTA), jijini Istanbul, Uturuki. Madrid ilishinda bao 3-0.
Mshambuliaji Didier Drogba wa Galatasaray, akipiga shuti kujaribu kufunga, huku akizongwa na Michael Essien wa Madrid.

ISTANBUL, Uturuki

Galatasaray inakabiliwa na kibarua kipevu kuweza kubadili uongozi wa mabao 3-0 iliovuna Madrid ikiwa nyumbabni Santiago Bernabeu wiki iliyopita – ili kufuzu nusu fainali ya michuano hii tajiri zaidi ngzi ya klabu duniani

WENYEJI wa Uwanja wa Turk Telecem Arena (TTA) jijini hapa, Galatasaray AŞ leo inajitupa dimbani hapo kuikabili Real Madrid ya Hispania, katika mechi ya marudiano robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Galatasaray inakabiliwa na kibarua kipevu kuweza kubadili uongozi wa mabao 3-0 iliovuna Madrid ikiwa nyumbabni Santiago Bernabeu wiki iliyopita – ili kufuzu nusu fainali ya michuano hii tajiri zaidi ngzi ya klabu duniani.

Mabao matatu – moja moja kutoka Cristiano Ronaldo, Karim Benzema na Gonzalo Higuain, yanawapa Madrid uhakika wa kufuzu nusu fainali ya 24 ya michuano ya klabu barani Ulaya – huku yakiwapa wakati mgumu ‘Gala’ waliye na mshambuliaji Didier Drogba.

Galatasaray inayonolewa na kocha Fatih Terim Iko katika harakati ya kubadili matokeo hayo kwa kuwachapa Madrid, ili kutinga nusu fainali yao ya kwanza ya michuano ya klabu Ulaya katika kipindi cha miaka 24.

Akizungumzia matarajio yake katika mechi ya leo Jumanne usiku, Mourinho alisema: “Kama tutafanikiwa kufunga bao, basi watapaswa kutufunga mabao matano ili kutung’oa, lakini katika soka nimeshaona matokeo ya kustaajabisha na kuacha midomo wazi, kwamba hakuna kitakachonishangaza leo.

“Istanbul ni mahali pagumu mno kucheza mechi utakavyo, wao watapambana hasa dhidi yetu. Tunapaswa kuingia mchezoni tukiwa makini mno, ambayo ndio njia pekee tunayopaswa kuitumia kucheza.

Kwa upande wa Galatasaray, kocha wake Fatih Terim, alikiri kuwa; “Mechi hii itakuwa ngumu mno kwetu.
“Wiki iliyopita, tulienda ugenini tukijua tungevuna matokeo ambayo yangeturejesha nyumbani tukiwa na la kujivunia, lakini bahati mbaya hilo halikutokea, licha ya nyota wangu kujaribu kucheza kwa ubora wao wote.

“Tunahitaji kuacha kufikiria na kutenda kwa hisia. Kama tutabadilika kutoka tulivyokuwa jijini Madrid, tunaweza kuwa tumetoka kule tukiwa tumefungwa, lakini mabao ya kipindi cha kwanza katika mechi ya nyumbani yakabadili hali ya mambo katika mechi,” alijipa moyo Terim.

Katika mechi nyingine leo, Malaga iliyoshangaza wengi hatua kwa hatua za michuano hii, itakuwa na kibarua kigumu kudumisha mshangazo huo, wakati itakaposhuka kwenye dimba la Signal Iduna Park jijini Dortmund kujiuliza kwa wenyeji Borussia Dortmund.

Baada ya sare tasa nyumbani La Rosaleda wiki iliyopita, leo inajaribu kupigana kuhakikisha inakuwa moja ya klabu tatu za Hispania katika nusu fainali ya michuano, huku Dortmund nao wakipanga kuwafuata Bayern ambao wako pazuri kuelekea hatua hiyo.

SuperSpot.com

No comments:

Post a Comment

Pages