Kinara wa ubora wa viwango vya tenisi duniani, Novak Djokovic, akilibusu kombe la ubingwa wa ichuano ya Monte Carlo Masters 2013, alilotwaa baada ya kushinda Rafael Nadal kwa seti 2-1. Fainali hiyo ilifanyika Jumapili jijini Monaco, Ufaransa.
Djokovic kushoto, akipozi kwa picha na mshindi wa pili wa Monte Carlo Masters 2013, Nadal, baada ya fainali hiyo na kukabidhiwa vikombe vyao.
Nadal kushoto akitoa neno la shukrani kwa waliohudhuria fainali hiyo, huku Djokovic akitabasamu akiwa na kombe la ubingwa wa Monte Carlo Masters 2013.
MONACO, Ufaransa
"Sikujua kama naenda kuwa sehemu ya mafanikio ya michuano hii mwaka huu. niliamua kukubali kucheza mashindano haya, na hivi sasa najiona kwamba nilifanya maamuzi sahihi mno katika maisha yangu ya michezo"
KINARA wa ubora katiika viwango vya dunia vya mchezo wa
tenisi, Novak Djokovic juzi alihitimisha mfululizo wa miaka minane wa nyota Rafael
Nadal kushinda michuano ya Monte Carlo Masters, kwa kumchapa na kutwaa ubingwa
huo katika fainali.
Djokovic nyota wa kimataifa wa Serbia, amempa kichapo cha
kwanza Nadal katika michuano ya Monte Carlo katika mechi 47, akilipa kisasi cha
mwaka jana alipoangukia pua katika fainali ya michuano ya Masters.
Nadal alishuhudia Djokovic, 25, akianza kwa kaaasi na
kushinda seti ya kwanza kwa 6-2 katika muda wa dakika 46, kabla ya kushinda 7-6
na kulala 7-1 katika seti ya mwisho.
Djokovic alikuwa akihaha kutokana na jeraha la enka
lililokuwa likimsumbua tangu raundi ya awali, lakini hakuonesha dalili za
kukwazwa na hali hiyo mchezoni na kupigana kuweza kumshinda hasimu wake huyo.
"Sikujua kama naenda kuwa sehemu ya mafanikio ya
michuano hii mwaka huu. niliamua kukubali kucheza mashindano haya, na hivi sasa
najiona kwamba nilifanya maamuzi sahihi mno katika maisha yangu ya michezo,"
alisema Djokovic.
Katika mechi hiyo ya kwanza baina yao tangu Nadal
aliposhinda fainali ya French Open Juni mwaka jana, Djokovic alielemewa katiika
seti ya kwanza akiwa nyuma kwa 5-0, huku Nadal akitisha na kuaminisha wengi
kuwa angeshinda fainali hiyo.
BBC Sport






No comments:
Post a Comment