HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

April 29, 2013

Redd’s yafanya kweli Miss Tarime


Na Mwandishi Wetu, Tarime

ILIONEKANA haiwezekani, lakini kwa sasa mambo yameiva pale kwa mara ya kwanza katika historia Redd’s Miss Tarime alipatikana toka kuanzishwa kwa mashindano ya Miss Tanzania.
 
Redd’s Miss Tarime wa kwanza kabisa ni Mariam Kalioko, ambaye aliwashinda washiriki wengine wote waliojitokeza na kuvikwa taji hilo, hivyo kupata fursa ya kuiwakilisha wilaya katika mashindano ya mkoa.
 
Kutokana na ushindi huo, Mariam alipata zawadi ya Sh 500,000 aliyokabidhiwa papo hapo pamoja na kupata fursa ya kusomea masomo ya kompyuta kwa muda wa mwaka mmoja.
 
Mshindi wa pili katika shindano hilo lililofanyika katika Ukumbi wa JJ, alikuwa ni Magreth Victor aliyeondoka na kitita cha Sh 300,000 pamoja na kupata fursa ya kusomea kozi ya kompyuta kwa mwaka mmoja.
 
Katika shindano hilo lililoambatana na burudani kibao, mshindi wa tatu alikuwa ni Adema ambaye aliondoka na Sh 200,000 pamoja na kupata pia fursa ya soma masomo ya kompyuta.
 
Akizungumza mara baada ya kuvikwa taji, Mariam alisema amejisikia faraja kubwa kwani amekuwa Redd’s Miss Tarime kwa mara ya kwanza kitu ambacho hakukitarajia.
 
“Nimejisikia faraja mno na nawaahidi wana Tarime wote kwamba sitawaangusha na nitahakikisha nafanya kweli na hatimaye kutwaa taji la Redd’s Miss Tanzania,” alisema.
 
Mratibu wa mashindano hayo, Grace Revocatus alisema amejisikia faraja kubwa kumpata Redd’s Miss Tarime kwa mara ya kwanza toka kuanzishwa kwa shindano la Miss Tanzania nchini.
 
Shindano la Redd’s Miss Tanzania kwa sasa linadhaminiwa na kinywaji cha Redd’s Original ambacho kinazalishwa na kusambazwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL).

No comments:

Post a Comment

Pages