MKURUGENZI
Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Magu, Naomi Nnko akishiriki kuimba na
wanakwaya wa kikundi cha Magu One Theatre (MOT), wakati wa maadhimisho ya Siku
ya Afya ya Macho Duniani yaliyofanyika juzi (19.4.2013) katika viwanja vya
Hospitali ya Wilaya ya Magu, mkoani Mwanza. (Picha na Emmanuel Ndege)
Baadhi ya
wazee wakazi wa Wilaya ya Magu wakiwa katika maadhimisho ya Siku ya Afya
Duniani yaliyofanyika katika viwanja vya Hospitali ya Wilaya ya Magu, baada ya
kufanyiwa upasuaji wa mtoto wa jicho ili kuwawezesha kuona tena. Kutoka kulia
ni Weja Mfalasi, Constantine Mgana na Bujingwa Ngelela.
MKUU
wa Wilaya ya Magu, Jacqueline Liana akisalimiana na baadhi ya wazee ambao
walifanyiwa upasuaji wa macho na kuwawezesha kuona tena katika maadhimisho ya
Siku ya Afya ya Macho Duniani yaliyofanyika katika viwanja vya Hospitali ya Wilaya ya Magu,
mkoani Mwanza.
MKUU
wa Wilaya ya Magu, Jacqueline Liana (watatu kutoka kushoto) akiwa katika Chuo
Cha Ualimu Mukidoma kilichoko wilayani humo, wakati wa ziara yake ya kukagua
miradi ya maendeleo. Wengine katika picha ni viongozi na wahadhiri wa chuo
hicho
MKUU
wa Wilaya ya Magu, Jacqueline Liana, akiteta jambo na Mkurugenzi wa hoteli ya
Bujora Point Swimming Pool & Lodge, Benjamin Mgonzwa, baada ya ufunguzi wa
ukumbi wa kisasa wa hoteli hiyo iliyoko Kisesa, wilayani Magu katika mkoa wa
Mwanza


No comments:
Post a Comment