HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

April 25, 2013

UHABA WA DAWA UNASABABISHWA NA WIZI MKUBWA WA DAWA KATIKA HOSPITALI ZETU NA SIO MSD

Mganga Mkuu Mkoa wa Singida Dakta Doroth Kijugu akitoa mada yake katika semina ya wadau wa huduma za dawa kuhusu mfumo wa Direct Deliver -DD iliyofanyika mjini Iringa kuhusu wizi wa dawa  katika Hospitali, Vituo vya Afya na Zahanati hapa nchini, Semina hiyo iliandaliwa -MSD

Mhariri wa Dira ya Mtanzania Saleh Mohamed akisisitiza jambo katika mada ya Utafiti wa Waandishi wa habari kuhusu mpango wa MSD wa DD.  Waandishi wengine ambao wameshiriki katika kuandaa mada hiyo ni pamoja na Florence Majani wa Mwananchi na Shabani Tolle wa ITV.
Picha ya juu na chini  ni washiriki wa semina ya wadau wa huduma za dawa wakiwa katika picha ya pamoja na Mwenyekiti wa semina hiyo  Bw. Edward Terry  Director Zonal Operations katikati mwenye miwani. 

Baadhi ya wafanyakazi wa MSD wakiwa katika maonyesho madogo ya vifaa vinavyotolewa na MSD.
 Pichani kulia ni kitanda cha kujifungulia. Zahanati nyingi hususani za vijijini zina tatizo la ukosefu wa vitanda hivyo.
Mwakilishi wa MSD Bw. Celestine Haule akijibu baadhi ya maswali ya washiriki wa semina ya wadau wa huduma za dawa katika semina ya DD ambayo imeandaliwa na MSD mjini Iringa.
Waandishi wa habari Florence Majani (kulia) na Saleh Mohamed  wakifuatilia kwa makini  mada mbalimbali zinazoendelea kutolewa katika semina ya wadau wa huduma za dawa mjini Iringa.

No comments:

Post a Comment

Pages