HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

April 30, 2013

Wabunge wasiotakiwa Bunge la sasa


Na Bryceson Mathias
Katika mkoa fulani ambako ushirikina umekithiri, baadhi ya wanandoa wenye hulka ya Analojia ya mapenzi, wamehusishwa na mapokeo ya mafundisho hasi kwamba, ukiona ndoa inaharibika basi jitahidi kumpa mwenzi wako nyama ya ulimi. Na kwa kupofuka mawazo,wengi wao humaliza mabucha ya nyama wakinunua ndimi za ng’ombe.
Uongo mwingine ambao jamii ya kundi hili hudanganywa nalo likadanganyika. Ni kutokana na kukosa maarifa, waganga wa kienyeji huwahadaa na kuwaambia wakatafuta Mjusi mwenye rangi ya  Blue na Nyekundu Shingoni ambaye, akiwa kwenye mawe akiona mtu huiinuainua kichwa kwa maana ya Ndiyo! N diyo yaani  (Yes. Yes Yes)’  
Inasemekana, waganga wakipelekewa Mjusi huyo.humkausha na kumsaga akawa unga, ambapo wanandoa au wapenzi wa kiume au kike, humuwekea kwenye chakula, Chai  au Uji, kwa Imani akinywa atamsikiliza, na lolote atakalosema, basi ataitikie kwa kutikisa kichwa kama Mjusi  Yes Yes Yes, bila maswali.
Wazee wabunge la leo, wamekuwa na tabia ya kutaka Vijana wa leo wenye upeo mkubwa wa kifikra na uwezo wa kuchambua na kuchanganua mambo; wamekuwa wakiwalisha maneno na kuwapotoa mawazo ili wawe kama wao wanaolala usingizi bungeni, na kuchezesha vichwa kama mijusi, wakati wao ni kizazi cha Digitali.
Wazee hawa wanaosinzia bungeni wakati mwingine udenda unawatoka bila kujielewi, ndio wale wanaotaka Bunge lisioneshwe  kwa sababu wataonekana wamelala, na wakati mwingine kuogopa kuonekana jinsi wanavyojikanyanga kwa hoja nyepesi, tofauti na za vijana zilizochambuliwa.
Hawa ndio waeneza Udini, nani achinje, na vyuoni wakitaka wanafunzi wachujwe kwa majina ya dini, Ukabila na nyadhifa za wazazi wao ndani ya Serikali!. Hao ndio ambao wanataka tangu mfagiaji awe Dini fulani, Kabila Moja,  wanaotoka Ukanda fulani au mtoto wa ndugu, ambapo Karani hadi Mkurugenzi ni wao.
Humo ndimo wamo wasiotaka kuwepo kwa vyama vingi kukuza Demokrasia, ingawa kwa uongo wataunda vyama na kuviua kwa hila ili kuihadaa dunia kuwa kuna Demokrasia, wakati ni uongo na unafiki wa mchana kweupe. Hao ndio watu wanaopenda kesi zihukumiwe kwa kurudia rudia na ving’ang’anizi wakubwa kama kupe.
Hao watataka wabunge wenzao wafukuzwe bungeni na adhabu ziendelee ili wapate kuwaongoza wenye kuchezesha vichwa kutokana na kula Unga wa mjuzi kwenye Chai, Uji, Maziwa au Chakula, na mbaya zaidi watataka hata wananchi wasihoji chochote kilicho haki yao, na akitokea kijana anayewatetea atawekwa kitimoto si Nyama adha.
Hao ndio ambao wamekosa mafunzo ya ulezi, ambapo bila hofu wala aibu, wanaweza kufyatua matusi yasiyo na heshima, hadi unashangaa kama katika familia zao kuna chembe ya Heshima japo ya kuombea maji ya kunywa majumbani mwao.
Tofauti na wabunge wanafundishwa wakaseme nini na kuingia na vikaratasi huku wakisoma, wabunge vijana wasiotakiwa ni kama  akina Joseph Mbilinyi, Tundu Lissu, Ezekiel Wenje, Godbless Lema, Higness Kiwia, Halima Mdee, Kabwe Zitto, Peter Msigwa, Moses Machali, David Kafulila, Felix Mkosamali, Deo Filikunjombe, Kangi Lugola, John Mnyika, Luhaga Mpina na wengineo.
 Aidha Vijana hawa wamefanya juhudi kuupata ubunge wao na kupiga mweleka wa Mende ambaye ameangusha Kabati,  huenda wangependa watoto wao warithi uongozi wao kama wa kifalme, hawatajisikia vizuri, ikitokea mahali kuna fujo na wao wametuliza fujo hiyo na wao wameshindwa, watazuliwa jambo kuwa amewachochea.
 0715933398

No comments:

Post a Comment

Pages