Baadhi ya washiriki wakifuatilia mada hiyo kwa umakini.
Ofisa Mtendaji mkuu wa TTCL Dkt. Kamugisha Kazauraakiwasilisha mada kwenye mkutano huo, kushoto ni Eng. Samuel D. Shila kutoka kampuni ya Service Consult Ltd na kulia ni Bw. Mringi Kitaly kutoka Msafiri Infrastructure and Mining Solution.
Dk Kazaura (kushoto) akipata maelezo kutoka kwa bi. Josephine Mwakapugi kuhusu huduma zitolewazo na TTCL.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa TTCL Dk. Kamugisha Kazaura akifafanua jambo kuhusu mkongo wa taifa wa mawasiliano kwa waandishi wa habari na wateja waliotembelea katika banda la TTCL, wakati wa kutano wa Bodi ya Usajili wa Makandarasi uliofanyika Mlimani City jijini Dar es Salaam.
Na Mwandishi Wetu
Ofisa mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) Dk. Kamugisha Kazaura ametoa mada kuhusu mkakati wa TTCL kusambaza mawasiliano ya kasi katika majengo nchini wakati wa mkutano wa bodi ya Usajili wa Makandarasi ( Contractors Registration Board (CRB) ambapo pia bodi hiyo ilikuwa ikiadhimisha miaka kumi na tano tangu kuanzishwa kwake.
Katika mkutano huo uliohudhuriwa na makandarasi takribani 800 kutoka sehemu mbalimbali hapa nchini, Dk. Kazaura aliwaeleza nia ya TTCL kusambaza mawasiliano ya kazi katika majengo mbalimbali hapa nchini na kuomba ushirikiano wa hali ya juu kutoka kwa makandarasi kujenga majengo ambayo yatakuwa yamewezeshwa tayari kuunganishwa na huduma za
mawasiliano ya kasi " Broadband Ready Buildings".
No comments:
Post a Comment