HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

May 31, 2013

BEN POL AANDAA VIDEO YA PETE

Na Elizabeth John

BAADA ya kupata maoni kutoka kwa mashabiki wake mbalimbali, msanii wa muziki wa RnB nchini, Benard Paul ‘Ben Pol’ anatarajia kuachia video ya ngoma yake ya ‘Pete’ inayofanya vizuri katika vituo mbalimbali vya redio.

Pete ni kati ya nyimbo ambazo zimemuweka pazuri msanii huyo na kumfanya aingie katika kategori tatu kupiti wimbo huo katika tuzo za Kilimanjaro mwaka huu.

Akizungumza na Habari Mseto jijini Dae es Salaam jana, Ben Pol alisema kutokana na maoni anayoyapata kwa watu tofauti ameamua kufanya haraka kushuti video ya wimbo huo ambapo kwasasa yupo katika hatua za mwisho.

“Namshukuru mungu kazi hii inafanya vizuri katika vituo mbalimbali vya redio na niliipa muda wa kutosha pasipo kuiandalia video, wapenzi wa Pete wakae mkao wa kula,” alisema.


Alisema mbali na kutamba na kibao hicho, pia anawaomba mashabiki wake waendelee kumpa sapoti katika kazi zake zinazofuata ambazo anatarajia kwamba zinakua ni moto wa kuotea mbali.

No comments:

Post a Comment

Pages