Na Bryceson Mathias
CHAMA cha Mapinduzi (CCM) kinahitajika kibadilike, hasa wakati huu ambao wananchi wana uelewa mpana kuhusu Haki zao, na akama hakitafanya hivyo, amini usiamini kwa mtaji wa Kero mbalimbali zinazowakabili wananchi nchi, mwaka 2015 kinaweza kulia na kusaga Meno.
Kulia na kusaga Meno kutatokana na hasira za wananchi na hasa wazee, ambao watoto wao walio wengi, wamekuwa wafuasi na wapenzi wa Vyama vya Upinzani, hivyo kutokana na Wimbi la Polisi kuwakamata kamata kila mara na kuwafunga ovyo; Wazazi hao wanachukizwa.
Maneno yasiyo rasmi ya Vijana vijiweni yanadai, Kamata Kamata na kushikiliwa na Polisi kila mara, kumetafsirika kunaasisiwa na Viongozi wa CCM ili kutiwasha na kupunguza nguvu na kuwafumba midomo, ambapo ndugu ambao wengi ni wana CCM, wanaudhika na kuichukia.
Tunakubaliani wazee wengi ni wafuasi wa CCM, hivyo wakikasiridhwa nyumba moja, ufahamu kuna ukoo wa pande mbili za mke na mume, ambapo iwapo nao ni wana CCM nao wakikasirishwa kwa namna hiyo, basi Chama kitakuwa kinajikaanga kwa mafuta yake.
Hivi karibuni Mbunge wa Viti Maalumu, mkoa wa Iringa, Chiku Abwao (CHADEMA),alimlipua Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi, akidai ndiye analiharibu Jeshi la Polisi nchini akimtuhumu ana litumia kufanya kazi za kisiasa.
Abwao ambaye alikuwa akichangia hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Mambo ya Ndani iliyowasilishwa bungeni na Waziri Emmanuel Nchimbi, ambapo alisema kuwa Lukuvi anatumia jeshi hilo kuwabambikizia watu kesi jimboni kwake Isimani.
Nukuu “Mheshimiwa Spika mara zote nimekuwa nikisema humu ndani kuwa sisi hatuna shida na Jeshi la Polisi bali kuna watu wanatumika kuliharibu Jeshi hilo na leo nitamtaja mtu huyo kwa jina ni Waziri Lukuvi,” alisema.
Abwao ambaye alikuwa akishangiliwa na Wabunge wenzake wa upinzani wakati anaanza kuchangia. Lukuvi hakuwepo ukumbini lakini aliingia ghafla na kuibuka utani kwa wabunge wa CCM wakisema, “Huyo kaja.”
Kama kinachodaiwa dhidi ya Polisi kutumika na viongozi ni kweli au siyo kweli, ifahamike kwamba, sumu inayoingia akilini mwa watanzania, dhidi ya matukio hayo, yatakuwa sababu kubwa mojawapo yakuwakasirisha watanzania kwenye chaguzi za mwaka 2014 na 2015.
Waswahiri husema, palipo na mzoga ndipo walipo kunguru; hivyo basi naonya na kushauri kwamba, Kamata Kamata na kushikiliwa kwa vijana na Polisi kila mara, kunatakiwa kuangaliwe upya na CCM, kwa sababu kupuuza matukio hayo, ni kilio 2014 nq 2015.
Kwa hali ya medani ya siasa inayojiri sasa, viongozi wa vyama vya upinzani, wamekuwa hawaogopi kukamatwa na Jeshi la Polisi wakiwemo vijana wao. Kwa namna hivyo Polisi baadaye itakuwa haiogopwi kama watu wasivyoogopa Joka linalochezewa na Kibisa.
Ni rai yangu Jeshi la Polisi, lijaribu kuepuka kuzoeleka na wananchi kunakotokana na kufanya vitendo vinavyolipunguzia hadhi Jeshi hilo, hasa pale linapofanya mambo ambayo hata Kipofu na asiyejua sheria, anabaini kuna ukiukwaji au mchezo mchafu.
Nitoe mfano; kutokana na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kutojichafua kwa matukio ya ovyo mbele ya wananchi. Jeshi hilo limekuwa likiheshimika sana.
Kwa msingi huo akitokea Kamanda wa JWTZ akasimama kutoa amri ya wananchi watekeleza Jambo fulani, watatekeleza haraka.
nyeregete@yahoo.co.uk 0713-933308.
No comments:
Post a Comment