HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

May 24, 2013

DAB, TRANSAFRICA ZAZINDUA USHIRIKIANO WA KIBIASHARA


 Meneja wa DAB barani Afrika, Carlo Fuccella, akifunua pazia maalum kama ishara ya uzinduzi wa ushirikiano wa kibiashara na Kampuni ya TransAfrica Water uliofanyika juzi jijini Dar es Salaam. DAB imeitangaza TransAfrica kuwa msambazaji mkuu wa bidhaa zake nchini Tanzania.
 Meneja wa DAB barani Afrika, Carlo Fuccella (kulia), akishikana mikono na Mkurugenzi Mtendaji wa TransAfrica Water, Tony Mwangi wakati wa hafla ya uzinduzi wa ushirikiano wa kibiashara baina ya kampuni hizo. Katika hafla hiyo hivi karibuni, DAB iliitangaza TransAfrica kuwa msambazaji mkuu wa bidhaa zake nchini Tanzania
 Baadhi ya waalikwa wakishuhudia zoezi la uzzzzinduzi huo.
 Mhariri wa Habari Mseto Blog, Salum Mkandemba (kushoto), akiwa na mpiga picha wa blog hiyo John Dande wakiangalia baadhi ya vifaa kwenye duka la kisasa la TransAfrika wakati wa uzinduzi huo.
 Mmoja wa waalikwa akiuliza swali kwa wafanyakazi wa kampuni hiyo kuhusu vifaa vilivyo katika duka hilo. 
Wawakilishi wa Kampuni za DAB na na TransAfrika Water, wakiwa katika picha za pamoja na Meneja wa DAB, Carlo Fuccella (wa tano kulia) na Mkurugenzi wa TransAfrica (wa tatu kushoto). 

DAR ES SALAAM, Tanzania

Meneja wa DAB barani Afrika, Carlo Fuccella, alisema kuwa ushirikiano huo utahakikisha Watanzania wanapata bidhaa zenye ubora wa hali ya juu na za kuaminika kutoka Italia na zitapatikana kwa bei nafuu inayoendana na ubora wake

KAMPUNI ya DAB Water Techology, imezindua ushirikiano wa kibiashara na Kampuni ya TransAfrica Water na kuwatangaza rasmi kuwa wasambazaji wakuu wa bidhaa zake nchini Tanzania.

Hafla ya kuzindua ushirikiano huo ulifanyika jijini Dar es Salaam katika Ofisi za TransAfrica Water, sambamba na uzinduzi wa pampu mpya za maji na vifaa vinavyotumika katika mifumo mbalimbali ya usambazaji maji majumbani, viwandani na mashambani.

Meneja wa DAB barani Afrika, Carlo Fuccella, alisema kuwa ushirikiano huo utahakikisha Watanzania wanapata bidhaa zenye ubora wa hali ya juu na za kuaminika kutoka Italia na zitapatikana kwa bei nafuu inayoendana na ubora wake.

“Tunafurahishwa sana ushirikiano wetu na TransAfrica Water na tuna imani kwamba
Bidhaa zetu zitapokelewa vema katika soko la Tanzania kwa kuwa zina ubora,” alisema Fuccella.

Fuccella aliipongeza TransAfrica Water kwa kufungua duka la kisasa lenye kiwango cha juu lenye bidhaa za bora, huku akiishukuru kwa kwa dhamira yao ya kuendeleza bidhaa na vifaa vya DAB.

Awali Ofisa Mauzo wa TransAfrica Water, Enock Ntilambungu, alisema kuwa, kampuni yake inajivunia ushirikiano wake na DAB, huku akiitaka serikali kupunguza tozo ya kodi kwa vifaa vya umwagiliaji, ili kuwawezesha wakulima kutekeleza sera ya kilimo kwanza.

No comments:

Post a Comment

Pages