Nahodha wa FC Bayern Munich ya Ujerumani, Phillip Lahm akiwa ameshikilia taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya, walilolitwaa jana usiku baada ya kuichapa Borussia Dortmund pia ya Ujerumani kwa mabao 2-1 katika fainali iliyopigwa kwenye dimba la Wembley jijini London.
Wachezaji wa Bayern Munich wakiendelea kushangilia ubingwa huo.
Wachezaji wa Bayern Munich wakishangilia baada ya filimbi ya mwisho.
Wachezaji wa Bayern Munich wakishangilia baada ya filimbi ya mwisho.
Mshambuliaji Robert Lewandowski wa Dortmund, akijaribu bila mafanikio kumtungua kipa Emmanuel Neuer wa Bayern.
Arjen Robben akijaribu kumfunga kipa wa Dortmund, Roman Weidenfeller. Hata hivyo shuti hilo laini lilimpiga usoni kipa huyo na Robben kushindwa kuipa timu yake bao.
Robben akijaribu kufunga kwa kutumia guu la kulia katika shambulizi jingine.
Robben akifunga bao la ushindi katika dakika ya 89 ya mtanange huo na kuipa timu ya Bayern ushindi uliowataza kuwa mabingwa wa Ulaya kwa mara ya tano katika historia ya klabu hiyo ya Allianz Arena.
Dimba la Wembley dakika chache kabla ya kuanza kwa mtifuano wa fainali ya Mabingwa Ulaya kati ya Bayern Munich na Borussia Dortmund zote za Ujerumani.
Kansela wa Ujerumani, Angela Merkel (wa pili kulia), akiimba wimbo wa taifa kabla ya kuanza kwa mtanange huo wa fainali kwenye Uwanja wa Wembley jana usiku.
No comments:
Post a Comment