Na Mwandishi Wetu
KAMPUNI ya Uwekezaji ya Afrika Kusini (ESG), imetenga dola
milioni 600 kwa ajili ya kuwekeza nchini katika ujenzi wa miradi mikubwa ya
barabara, Bandari, reli pamoja na kuongeza uzalishaji wa nishati ya umeme.
Akizungumza na viongozi wa taasisi za serikali katika
mkutano uliofanyika jijini Dar es Salaam juzi, Mwenyekiti wa ESG, Simon Haliva
alisema Tanzania inavivutio vingi ambavyo kama vikiendelezwa vinaweza kuleta
maendeleo makubwa kwa wawekezaji na taifa kwa ujumala.
Alisema kutokana na miradi mbali mbali aliyoelekezwa na
viongozi hao atajitahidi kuifanyia kazi ili kuhakikisha anaanza mpango huo
haraka ili kuongeza uzalishaji nchini.
“Mimi na wenzangu tutakaa na kuipitia kwa makini miradi hii
mliyotuarika na baada ya muda mfupi tutarudi ili kuwekeana mikataba mbali mbali
ya miradi mlionayo kwaajili ya kuifanyia kazi” alisema Haliva.
Naye Afisa Mwandamizi wa uwekezaji kutoka Kituo cha
uwekezaji Tanzania (TIC), Brendan Maro alibainisha kuwa ujio wa wawekezaji hao
nimafanikio ya jitihada zai za kila siku katika uwajibikaji wa kuhakikisha
miradi mbali mbali inawezeshwa na kuleta tija kwa taifa.
“Tunaamini wawekezaji watakuja kwa wingi kwa kuwa wengi
wameonyesha moyo wa kutusaidia kwa kushirikiana na sisi katika shughuli mbali
mbali za maendeleo kupitia miradi mbali mbali” alisema Maro.
No comments:
Post a Comment