HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

May 29, 2013

KASEBA APANIA KUMKALISHA MMALAWI

Na Elizabeth John


BONDIA wa ngumi za mateke ‘Kick Boxer’ Japhet Kaseba amesema amejipanga kuweka rekodi nzuri katika tasnia hiyo kwa kumchapa Mmalawi, Rasco Chimwanza katika pambano lao la kuwania ubingwa wa Afrika Mashariki na Kati linalotarajiwa kuchezwa Juni 8, mwaka huu.



Akizngumza na Habari Mseto jijini Dar es Salaam, Kaseba alisema anajua kama bondia huyo ni nyota katika tasnia hiyo, lakini kutokana na maandalizi aliyoyapata atahakikisha anaweka heshima katika ngumi za mateke.

“Namshukuru mungu nina afya nzuri hadi sasa na naendelea na mazoezi kwajili ya pambano hilo naomba Watanzania wajitokeze kwa wingi katika ukumbi huo wa DDC Magomeni,” alisema Kaseba.

Naye Katibu Mkuu wa Oganizasheni ya ngumi ya za kulipwa Tanzania (TPBO), Ibrahim Kamwe alisema maandalizi ya pambano hilo yamekamilika, na tayari wamemtumia nauli Mmalawi huyo na kwamba anategemea kuingia nchini Juni 5.

Alisema TPBO imemtengenezea mazingira mazuri ya ushindani, Kaseba na kwamba wanategemea atafanya vizuri katika pambano hilo kutokana na maandalizi ambayo anaendelea kufanya.




No comments:

Post a Comment

Pages