HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

May 05, 2013

KMKM MABINGWA LIGI KUU YA GRAND MALT ZANZIBAR

 Waziri Asiye na Wizara Maalum wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Machano Othman akimkabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya sh. milioni 10 nahodha wa timu ya KMKM, Maulid Ibrahimu baada ya kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Grand Malt huko Zanzibar. (Na Mpiga Picha Wetu
 Wachezaji wa timu ya KMKM wakiwa katika picha ya pamoja na kombe lao wakishangilia ubingwa wa soka wa Ligi Kuu ya Soka ya Grandmalt huko Zanzibar.
Timu ya KMKM wakiwa pamoja na kocha wao Ally Bushiri wakishangilia ubingwa wa Ligi Kuu ya Soka ya Grand Malt huko Zanzibar.

Na Mwandishi Wetu, Zanzibar

MABINGWA wapya wa Ligi Kuu ya Grand Malt, KMKM imesema itahakikisha inafanya kweli katika mashindano mbalimbali ili kudhihirisha umma kuwa, kinywaji hicho hakikukosea kuidhamini ligi hiyo.

Akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi washindi zawadfi iliyofanyika kwenye hoteli ya Zanzibar Ocean View, Afisa Michezo wa KMKM, Ramadhan Hassan ‘Mabio’ alisema hilo watalifanya pamoja na pia kuilinda heshima ya timu.

“Timu yetu ni moja kati ya zile kongwe hapa Tanzania, hivyo napenda kuahidi kwamba tutafanya kila iwezalo ili kuwafanya wadhamini wetu wajisikie furaha kwa kushinda kwa mechi tutakazocheza.

“Kwa muda mrefu soka la Zanzibar lilikuwa limeyumba kutokana na kukosa mdhamini, ila kwa sasa tunapenda kuwashukuru Grand Malt kwa kudhamini Ligi Kuu ya Zanziobar,” alisema.

Maneno hayo yaliungwa mkono na wadau mbalimbali wa soka visiwani hapa, ambao walisema udhamini wa Grand Malt umesaidia kwa kiasi kikubwa kuinua soka la Zanzibar.

Naye kocha wa KMKM, Ally Bushiri alisema kwa sasa anahakikisha anaiandaa timu kwa ajili ya mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

“Tunashukuru kwa kuwa mabingwa wa Ligi Kuu ya Grand Malt na sasa tunachofanya ni kutazama mbele zaidi,” alisema.

Ligi Kuu ya Zabnzibar kwa sasa inadhaminiwa na kinywaji kisicho na kilevi cha Grand Malt, ambao wameidhamini kwa misimu mitatu.

No comments:

Post a Comment

Pages