Baadhi ya majeruhi wakiwa wameanguka chini kufuatia
shambulio la bomu lililofanywa na mtu asiyejulikana ambapo zaidi ya watu 40
wamejeruhiwa na wengine watatu hali yao ni mbaya; tukio hilo lilitokea katika
ibada ya uzinduzi wa kanisa la Mtakatifu Joseph lililoko kata ya
Olasiti, mkoani Arusha leo.(Picha na Ferdinand Shayo)
Baadhi ya majerui wakiwa nje ya kanisa wakisubiri msaada wa kupelekwa hospitali.
Na Mwandishi Wetu
Bomu
limelipuka majira ya saa 5 leo asubuhi katika uzinduzi wa Parokia mpya ya
Olasiti, Jijini Arusha wakati Askofu Mkuu Josephat Louis Lebulu na Balozi wa
Baba Mtakatifu nchini, Askofu Mkuu Francisco Montecillo Padilla wakiwa wamejiandaa kuanza
maadhimisho ya misa ya kutabaruku kanisa hilo kwa kuwabariki waumini hao tayari
kwa ibada.
Taarifa za awali
zilizothibitishwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas zinasema
kuna majeruhi zaidi ya 30, lakini wanne walikuwa na majeraha makubwa, na
amewataka wananchi kutoa ushirikiano kuweza kuwabaini waliorusha na/au kutega
bomu kwenye eneo hilo la Ibada.
Akiahirisha Ibada hiyo
Vicar General wa Jimbo Katoliki la Arusha Padre Simon Tengesi aliwataka
wakristo wote kuondoka eneo hilo na uzinduzi huo umeahirishwa hadi pale
itakapotangazwa tena, na watu wameondoka eneo hilo ili kuruhusu vyomvyo vya
ulinzi na usalama viweze kuanza uchunguzi.
Chanzo chetu cha habari
kinasema eneo lilipolipuka bomu kuna damu nyingi na watu wamejeruhiwa sehemu
mbalimbali za mwili, Tutaendelea kuwajuza zaidi.
No comments:
Post a Comment