Watoto pia
walishiriki kwenye zoezi la upandaji miti.
Zoezi la upandaji
miti liliendeshwa mitaa mbalimbali ya Kilimahewa.
Wakazi wa Kilimahewa wakichangamkia zoezi la
kupanda miti.
Wana SVG wakijiandaa
na zoezi la upandaji miti 1,500.
SVG yatimiza mwaka mmoja yapanda miti zaidi ya
1,500.
Salasala Vision Group (SVG), ni kikundi cha wakazi wa
salasala Kilimahewa wapenda maendeleo kichoanzishwa mwaka 2012. SVG ilianzishwa ikiwa na malengo ya kuleta
maendeleo ya kijamii, kiuchumi, kiutamaduni na ulinzi kwa maeneo ya Salasala
Kilimahewa.
Tangu SVG ilipoanzishwa mwaka jana, kundi hili limeweza
kutekeleza mambo mengi katika mwaka mmoja; Kuanzisha ulinzi shirikishi katika
maeneo ya Salasala kilimahewa, Kutengeneza uwanja wa michezo, kuchangia mavazi
rasmi ya waendesha bodaboda, Kuanza kutoa mikopo kwa wanachama wa SVG, Kuendeleza mahusiano na makundi mengine yenye
malengo yanayoshabihiana na SVG.
Katika kuazimisha mwaka mmoja, wanachama wa SVG wamepanda
miti zaidi ya 1,500 katika maeneo yanayozunguka salasala kilimahewa. Zoezi hili
endelevu linatarajiwa kuendelea mwezi wote wa Mei na kufikia zaidi ya miti
2,000 kupandwa.
No comments:
Post a Comment