HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

May 06, 2013

WALIOKUFA KATIKA MLIPUKO ARUSHA WAFIKIA WATATU

Takriban watu watatu wamekufa kwenye mripuko wa bomu Jumapili asubuhi katika kanisa Katoliki la Olasiti nje kidogo ya mji wa Arusha, Tanzania.
Kanisa Katoliki jipya la Olasiti

Kwa mujibu wa Padri Festus Mangwangi ambaye ni paroko msaidizi wa kanisa katoliki jimbo la Arusha, mripuko ulipotokea walikuwa tayari kubariki maji kwa ajili ya uzinduzi wa kanisa, shughuli iliyokuwa ikiongozwa na balozi wa Papa Francis.Wengine kadhaa walijeruhiwa huku balozi wa papa na watawa waliokuwa katika shughuli hiyo maalumu ya kuzindua parokia mpya ya mtakatifu Yosefu walinusurika.


Hata hivyo Padre Mangwangi ameiambia BBC kuwa taarifa walizonazo muda mfupi baada ya majeruhi kukimbizwa hospitali, kuna watu watatu kati yao waliofariki na wengine wanapatiwa matibabu katika hospitali ya Mount Meru mjini Arusha.

Taarifa moja inasema watu kama 80 walijeruhiwa.
Watalaalamu wa miripuko na polisi wanaendelea na uchunguzi kuhusiana na mlipuko huo.

Bado hakuna taarifa ya chanzo cha mripuko au kama kuna mtu au kundi lilohusika.

Lakini msemaji wa polisi alieleza kwamba wanashuku kuwa mripuko ulisababishwa na bomu.
Hili ni shambaulio la kwanza la bomu nchini Tanzania japokuwa mwaka huu pia kulikuwa na tukio la mauaji ya Padre wa kanisa hilo visiwani Zanzibar, ambaye alipigwa risasi wakati akiwa anajiandaa kuingia .

No comments:

Post a Comment

Pages