Na Bryceson Mathias
WAJAWAZITO wa Hembahemba Kata ya Njoge Wilaya ya Kongwa, Wameikaba Serikali na kuitupia Lawama kwa kushindwa kuwapatia Madawa na wafanyakazi hivyo kulazimika kufuata Huduma ya Uzazi Kilomita 15, hali wanayo Zahanati waliyojenga kwa nguvu zao.
Hayo yamesemwa na Wajawazito hao Jumatano, Mei 8, Mwaka huu wakiwa njiani kwenda Kata ya Njoge kufuata huduma hiyo, Ingawa ahadi ya Serikali ilikuwa wananchi waboresha Vyumba Vinne kati ya 10 na kujenga Choo, halafu wapelekewe Madawa na Muuguzi.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti wanawake hao waliokataa katakata wasipigwe picha walisema, wanashindwa kuielewa Serikali kutotimiza ahadi hiyo kiasi cha akina wengi wasio na uwezo usafiri, kujifungulia njia wanapoelekea Kata ya Njoge kufuata huduma hiyo.
Kaimu Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji), Basira Nyalus (CCM), alikiri kuwepo kwa tatizo hilo na kusema, “Awali aliambiwa na Uongozi wake wa juu awahamasishe wananchi vijengwe vyumba vinne na Choo wapate huduma ya Muuguzi, lakini pamoja na kufanya hivyo kuko kimya”.
Kwa Upande wake Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Kata ya Njoge Maiko Mhahilidze licha ya kulalamikia udanganyifu huo, pia alililalamikia Ubovu wa Barabara na kuhoji, wanakusanya Ushuru wa Mazao kwa mwezi Laki Sita zinakwenda wapi?.
Hata hivyo wananchi hao kwa hasira walitaka kuvunja kizuizi cha Mazao wakidai, tangu 2009 ilipofunguliwa Amana (‘Account’) ya Sh. Laki Moja, wanajiuliza huo ushuru wa Sh.Laki Sita unaokusanywa kwa siku tangu 2009, mbona edha fhazionekani kwenye Amana, ziko wapi?.
Aidha walisema, wanashangaa kwa nini hawapati Ruzuku ya asilimia 20% toka Halmashauri tangu enzi ya Uongozi wa Mwenyekiti Elieneus Mhada na Mtendaji Mariam Simule (Dada wa Naibu Spika wa Bunge Job Ndugai, waliong’olewa na wananchi kwa kukataa kumpokea Mganga wa Kienyeji (Lambalamba).
No comments:
Post a Comment