NA DENIS MLOWE, IRINGA
KATIBU wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Iringa Vijijini, Sule Masanguti, amethibitisha kukamilika kwa hatua ya uchukuaji na urejeshaji wa fomu za kuomba kuteuliwa kugombea ubunge wa Jimbo la Isimani baada ya mchakato huo kuanza tarehe 17 mwezi huu.
Masanguti amesema kuwa zoezi limeenda vizuri na waombaji wote waliochukua fomu jumla ya 18 wamerejesha fomu zao kama ilivyopangwa.
Amesema kuwa kwa mujibu wa taratibu za chama, wagombea hao sasa wataendelea na hatua inayofuata ya kupigiwa kura za maoni kwenye kata zote za jimbo hilo kesho tarehe 19 katika kata 13.
Orodha ya wanachama waliochukua na kurejesha fomu wakiongozwa na mfanyabiashara maarufu nchini Tanzania Fred Fabian Ngajilo aliyekuwa mpinzani wa Lukuvi, Festo Kiswaga wengine ni Asakwe Lameck Widambe mfanyabiashara maarufu mkoani Iringa Arif Ally Abri.
Aidha aliwataja waliochukua fomu na kurudisha kuwa ni Eng. Sebastian Antony Kiyoyo, Dr. Tumaini Godwin Msowoya, Watende Gwerino Kiyagi, Lazaro Francis Ngwila, David Evance Komba na Thobias Karlo Mwilapwa
Wngine ni Tito Maulilio Cholobi, Emmanuela Kaganda Mtatifikolo, Claudio Francis Nzwaga, Josephat Gwelino Msambwa , Elias Lupituko Migodela Kazikuboma, Egidy Stanslaus Mkolwe, Dr. Abdallah Suleiman Lusasi na Tedson Johansery Ngwale
Katibu Masanguti ameongeza kuwa chama kimejiandaa kuhakikisha mchakato wa kura za maoni unafanyika kwa amani, uwazi na kufuata taratibu zote zilizowekwa na Chama Cha Mapinduzi.
Amesisitiza kuwa hatua hii ni muhimu katika kupitisha mgombea mmoja atakayewakilisha CCM katika uchaguzi mkuu ujao, na akawapongeza wanachama wote waliojiorodhesha kwa kuonesha utayari wa kuleta maendeleo katika Jimbo la Isimani.






No comments:
Post a Comment