HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

May 27, 2013

WASEMAVYO WANANCHI DHIDI YA KEJELI ZA NKAMIA KWA MCT, TEF NA WAANDISHI


Juma Nkamia, Mbunge wa Kondoa Kusini

Na Byceson Mathias

Mei 25, mwaka huu, niliandika makala iliyobeba mahudhuhi ya swali kuwa; kama Mungu angemteua Mbunge wa Jimbo la Kondoa Kusini, Juma Nkamia (CCM) kugawa baraka na haki za viumbe, je wanahabari wangepata?

Yafuatayo ni maoni ya mmoja na majibu ya wananchi kati ya wengi, wanavyoona umuhimu na msaada wa wandishi kwa wao kama Walalahoi, Jamii, Taifa na Kimataia.   

“Hello Bryceson! Nimesoma makala yako imuhusuyo Juma Nkamia kuhusu kile alichokisema au kulalamikia vyombo viwili vinavyoratibu shughuli zenu za uandishi wa habari.

 Binafsi nikiwa mtu wa kawaida natambua wazi kazi za vyombo hivyo vya Baraza la Habari (MCT) na kile cha Jukwaa la Wahariri (TEF), vimebadilisha sura ya Tanzania kuelekea demokrasia. Lakini hata mtu angekuwa kipofu angenusa japo manukato ya vyombo hivyo viwili.

Juma Nkamia si mwandishi wa habari, yule ni mtangazaji wa mpira! Kutangaza mpira ni upenzi wa mpira kila mtu anaweza kutangaza hata kama hajaenda shule! 

Ni mwandishi gani anaweza kutoa lugha ya matusi akiwa bungeni kama alivyosema Nkamia hivi karibuni?

Na kama ni mwandishi basi aliingia akiwa kama mpelelezi! Kazi za wapelelezi zinajulikana na hawa ndio kila siku huwajibika kutoa hata siri zenu binafsi za nyie waandishi!

 Lakini pia ukisikia mwandishi ameingia kwenye siasa za chama tawala (CCM ), tena kwa kuteuliwa ghafla 'bin-vuu' hawezi kuleta mchango wowote iwe ni kwa waandishi wenzake achilia mbali tasnia na wananchi.

Hilo ni janga! Ebu angalia leo Juma Nkamia unamsikia tena japo kwa ubunge wake? 'Yupoyupo' tu! Kuna wakati alitangaza eti atarudi kushika chaki akiwa mbunge! Ni uwongo mtupu kazi zao ni za kutumwa! Hasa kuharibu na kudhoofisha kazi za wengine hasa za kupigania maendeleo!

 Juma Nkamia hastahili kuwa Mbunge maana kazi za mbunge kama zilivyoainishwa yeye yupo yupo tu! Ni bahati mbaya saana kwamba amekuwa mbunge wakati wananchi walishabadilika kimtazamo na kifikra kwamba hawadanganyiki na pia yeye kurudi kwenye kiti cha ubunge 2015 litakuwa janga.

Lakini shida ya elimu ya kuungaunga ndio hiyo! 

Mfano mdogo tu ni mwandishi mzoefu ndugu Tiddo Muhando alipoletwa nchini aende kwenye siasa ambapo kama angekubali kwenda kwenye siasa hizo leo hii angekuwa janga ,lakini weredi wake na nguvu aliyonayo kutetea uandishi wa habari ulomjengea heshima kubwa, yaliyomukuta kila mtu anajua.

Kufanya kazi ya uandishi ukiwa na njaa na ubinafsi huwezi kuleta ufanisi wa kuiandika habari ama kuitangaza! Si umeona yaliyomukuta mwandishi wa staili hiyo kule Mtwara?

 Ni aibu Juma Nkamia kuropoka maneno yale ya shutuma dhidhi ya vyombo hivyo! Utaona tu nguruwe mwenye njaa! Hivyo visenti vya ubunge vinamzingua saana na kujiona ameshafika! 

Angevipata wapi kati maisha yake? Si anajua asipojipendekeza kwa kulamba makanyagio ya viatu vya watawala hawezi tunukiwa kwa mengine?

Ni kibaraka wa serikali aliyetokea kuwepo aliyetayari kuona nyumba ya udongo ya baba na mama yake ikizama kutokana na mafuriko ati tu kwa kuwa yeye yupo mlimani kwenye nyumba ya ghorofa! 

Na ninyi waandishi msitangaze habari zozote zimuhusuzo yeye na ikiwezekana mtangaze ufanisi wake duni wa ubunge ili ajue kwamba vyombo hivyo alivyovidharau vyaweza kumpandisha chati au kumshusha!

Lakini zaidi ya yote nachelea kuamini kama kuna mwandishi yeyote aliyegeukia siasa akatetea waandishi wa habari! Si yule Betty Mkwasa si alishafukuza waandishi wa habari? Si alikuwa
mwandishi wa habari yule, sasa leo yako wapi? 

Kuwapata akina Tiddo ni kazi ngumu sana. 

No comments:

Post a Comment

Pages