HABARI MSETO (HEADER)


June 06, 2013

AMIN: BAADA YA TUZO ZA KILI NAACHIA NGOMA YANGU MPYA

Na Elizabeth John
MKALI wa muziki wa kizazi kipya nchini kutoka nyumba ya kukuza vipaji Tanzania (THT), Amin Mwinyimkuu ‘Amin’ amesema anasubiri tuzo zitolewe kwa wasanii ambao wameingia kwenye kinyang’anyiro cha Kilimanjaro Music ili aweze kuachia ngoma yake mpya.

Wasanii kutoka THT ambao wameingia kwenye tuzo mwaka huu ni pamoja na Barnaba, Linnah, Recho, Ally Nipishe na Makomandoo.

Akizungumza na Habari Mseto jijini Dar es Salaam, Amin alisema kwasasa hawezi kuachia kazi yake mpya inayokwenda kwa jina la ‘Nipoze roho’ kutokana na kwamba wapenzi wa muziki huo kwasasa watakua bize na upigaji kura.

“Kwasasa mashabiki hawataangalia kitu kipya, wengi wanataka kujua msanii gani kashinda kwenye kinyang’anyiro gani na sio kuangalia msanii yupi katoa wimbo mpya,” alisema Amin.

Amin aliwataka wapenzi wa kazi zake wakae mkao wa kula kwaajili ya kukipokea kibao hicho ambacho anaamini kitaanza kusikika baada ya kumalizika kwa tuzo hizo.

Amin kwasasa anatamba na kibao chake cha ‘Ni wewe’ ambacho kinafanya vizuri katika tasnia hiyo.


No comments:

Post a Comment

Pages