Na Elizabeth John
MWANADADA anayeng’ara katika tasnia ya muziki wa
taarabu, Joah Kassim kutoka kundi la T-Moto amesema amegeukia tasnia ya filamu ili
kuonesha kipaji chake kwa mashabiki.
Akizungumza jijini Dar es Salaam, Joah
alisema ameamua kufanya hivyo ili kuonesha kipaji chake na kwamba yeye ni
msanii anajua nini anachokifanya katika fani hizo ambazo anauhakika anafanya
vitu ambavyo vinapendwa na jamii.
“Mimi kama msanii anatakiwa kuonesha kipaji
changu, filamu hii ni ya kwanza kucheza, nimecheza na mhogo mchungu, najua
wasanii wa filamu wakiiona hii watanitafuta kutaka nicheze filamu zao, nina
uhakika na nilichokifanya ndani yake,” alisema.
Joah aliwataka wapenzi wa filamu nchini,
kumpokea vizuri katika tasnia hiyo pamoja na kumpa sapoti katika kazi zake.
Kundi la T-Moto Taarabu kwasasa wanatamba na
kibao chao cha ‘Domo la Udaku’ ambacho kinafanya vizuri katika tasnia ya muziki
huo na pia wanajiandaa kukamilisha kazi yao mpya inayojulikana kwa jina la
‘Kuna mungu sio miungu’.
No comments:
Post a Comment